Askari mmoja wa jeshi la wananchi ameuawa kwa kupigwa risasi huku wengine wanne wa jeshi la polisi wamejeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa tanga bombo kufuatia mashambilizi ya kurushiana risasi katika mapango kati yao na vikundi vinavyodaiwa kuwa vya kigaidi.
Habari kutoka katika eneo la tukio zinadai kuwa vikundi hivyo vilikuwa ndani ya mapango huku askari wakiwa nje hatua ambayo imedaiwa kuwa majibizano ya risasi yalisababisha askari wa jeshi kupigwa ya tumboni na kuwahishwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa tanga bombo lakini baadae alifariki Dunia.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na ITV wameingiwa na hofu kufuatia tukio hilo huku baadhi yao wakidai kuwa wanashindwa kutoka katika nyumba zao kwa kuhofia usalama wao kufuatia milio ya risasi katika eneo la amboni hasa nyakati za usiku .
Hata hivyo kamishna wa Polisi -Operesheni na mafunzo Paul Changonja akielezea tukio hilo amekiri kuwa askari wake watatu na mmoja wa jeshi la wananchi wamejeruiwa kwa risasi wakati askari wake walipoingia katika mapango hayo ndipo mmoja kati ya wanakikundi hao aliporusha risasi na kuwajeruhi askari.
Hata hivyo jitihada za ITV kwenda katika eneo la tukio ziligonga mwamba baada ya askari polisi wa kikundi cha (FFU) kuweka ulinzi na kudai kuwa hatakiwi mwandishi wa habari kwenda katika eneo hilo huku mganga mkuu wa mkoa wa tanga Dr,Asha Mahita naye akitoa maelezo kama hayo kuwa waandishi wazuiwe wasiingie katika wodi ya galanosi kwa ajili ya kuwaona askari waliojeruhiwa.
Post a Comment