Safari ilianzia mitaa ya Kariakoo katikati ya Dar es Salaam.. alafu ikaenda mpaka Tandika, Temeke na mwisho kabisa ikawa maeneo ya Ilala.
Staa wa Muziki TZ ambae usiku wa June 13 2015 aliingia kwenye headlines kubwa baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya Tuzo SITA kuonesha jinsi ambavyo watu wake mtaani wamemkubali kwenye ujio wake mwingine baada ya kimya cha muda mrefu.
Ali Kiba ni mshindi pia wa Tuzo za Watu 2015 kwenye nafasi ya msanii wa kiume anayependwa.. YES, niko nae leo tena.. kaingia zake mtaani na akaona njia poa ya kukutana na watu wake ni kuingia katika daladala na kupiga story na kila shabiki wake wa nguvu aliyekutana nae humo.
Post a Comment