Featured

    Featured Posts

MAMA DIAMOND PLATNUMZ AFYA YAKE YATENGAMAA...ARUDI TOKEA INDIA SALAMA

Thank you God! Neno pekee unaloweza kusema ni Mungu mkubwa baada ya kusikia taarifa kwamba mama mzazi wa Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’, amerejeshwa Bongo kutoka India ambapo afya yake imetengemaa, Ijumaa Wikienda lina kitu kamili.
Mama mzazi wa Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’ akirejea kutoka India.
Habari kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya familia ya jamaa huyo, kililieleza gazeti hili kwamba, tayari  Sandra amesharejea katika hali yake ya kawaida na ndiyo maana akarudi Bongo baada ya kulazwa hospitalini nchini India kwa kusumbuliwa na ugonjwa wa kupooza.
Mwanafamilia huyo alisema kwamba, Diamond na mama yake walirejea nchini wikiendi iliyopita baada ya kufanyiwa matibabu ya kina na madaktari kujiridhisha kwa hali ya juu dhidi ya afya yake ambapo waligundua hali aliyonayo kwa sasa imetengemaa hivyo wakamruhusu kurejea kuungana na familia yake.
Habari zilieleza kuwa kwa sasa bimkubwa huyo yupo fiti na anaendelea na mazoezi ya kawaida huku akimalizia dawa alizopewa na wataalam hao wa afya.
Mama na mwana wakiwa ni wenye furaha baada ya kukutana tena.
“Mama amerejea juzikati kutoka kwenye matibabu nchini India alikokuwa amepelekwa, hivyo tunamshukuru Mungu sasa anaendelea vizuri na afya yake kwa jumla inaridhisha ingawa ana programu ya kufanya mazoezi mepesi ili aweze kuimarika zaidi ya vile alivyokuwa awali.
“Pia kuna dawa ambazo alipewa kwa ajili ya kumpatia nguvu zaidi,” alisema mmoja wa wanafamilia kwa ombi la kutotajwa gazetini.
Ijumaa Wikienda lilifika nyumbani kwa mama Diamond ambapo lilihakikishiwa kwamba bimkubwa huyo alikuwa ndani amelala na Diamond yupo nchini Afrika Kusini kikazi.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana