MENEJA Uzalishaji wa filamu ya Mbwa Mwitu ya Kajala Masanja, Abdul Ally ‘Mangi’ amefunguka kuwa Kajala amezungumza uongo kwa kusema yeye ndiye aliyeingia mitaani na kuwatafuta vijana walioigiza kwenye filamu hiyo.
Meneja Uzalishaji wa filamu ya Mbwa Kajala Masanja, Abdul Ally ‘Mangi’.
Kajala alifunguka kauli hiyo hivi karibuni katika Kipindi cha Take One kinachorushwa na Clouds TV, alipokuwa akizungumzia kazi zake za sanaa kisha kusema yeye ndiye aliyewatafuta vijana wa uswahilini walioigiza sinema hiyo.
Staa wa filamu Bongo, Kajala Masanja akihojiwa na mwandishi.
“Mwanzo niliona kwenye filamu yenyewe, nikanyamaza lakini kwa hili la kipindi sikupenda na hata nilipojaribu kuongea naye alinidharau na kunipa vitisho vya kutofanya naye kazi,” alisema Mangi.
Alipotafutwa Kajala, hakupokea simu lakini alipotafutwa meneja wake, Leah Mwendamseke ‘Lamata’, alisema Mangi si mkweli hao watu walitafutwa na Kampuni ya Kajala Entertainment.
Alipotafutwa Kajala, hakupokea simu lakini alipotafutwa meneja wake, Leah Mwendamseke ‘Lamata’, alisema Mangi si mkweli hao watu walitafutwa na Kampuni ya Kajala Entertainment.
Post a Comment