Featured

    Featured Posts

BSS 2015: KILICHOFICHWA NYUMA YA PAZIA CHAFICHUKA ...SOMA HAPA

MASHINDANO ya Bongo Star Search (BSS) 2015, wikiendi iliyopita yalifikia tamati huku historia ya kwanza ikiwekwa na kijana mwenye umri wa miaka 19 tu, Kayumba Juma aliyeibuka kidedea kwa kuwatupa wenzake 6 waliofaulu kuingia fainali na licha ya shughuli hiyo kumalizika salama, lakini kilichojificha nyuma ya pazia kimefichuka.
1Mshindi wa Shindano la Bongo Star Search 2015 (BSS), Kayumba Juma (katika), akiwa ameshikilia fedha zake muda mfupi baada ya kuibuka kidedea kwenye fainali hizo zilizokuwa zikifanyika katika Ukumbi wa King Solomoni uliopo Namanga jijini Dar es Salaa.
Fainali hizo zilifanyika Oktoba 9, mwaka huu kwenye Ukumbi wa King Solomon uliopo Ada Estate, Kinondoni jijini Dar huku zikishuhudiwa na maelfu ya wakazi wa jiji, burudani zilikuwa kibao siku hiyo ambapo zilianza saa 3: 30 usiku zikifunguliwa na mkali wa miondoko ya R&B, Bongo, Bernard Paul ‘Ben Pol’.
WASHIRIKI WAANZA
Baada ya Ben Pol kufungua ukurasa huo, kete ya kwanza kwa washiriki ilianza kwa kumdondokea mshiriki kutoka Mwanza, Angel Mary Kato aliyeonesha manjonjo yake akimpisha Kayumba Juma ambaye aliingia na Wimbo wa Christian Bella huku akipata shangwe nyingi kutoka kwa mashabiki waliomtunza fedha.
20
Madam Rita akifuta machozi muda mfupi baada ya kumkabidhi mshindi kitita cha shilingi milioni 50.
Baadaye, Nasibu Fonabo akichukua nafasi ya tatu kwa kufungua jukwaa hilo, tena akitumia gitaa huku Kelvin Geryson akiingia kwa makeke mengi na kumpisha Frida Amani ambaye alikuwa mshiriki kutoka Kaskazini.
Jackline Kakengi kutoka Bukoba alitoka na kuacha washiriki wenzake wakisonga mbele na kuunda Tano Bora.
LAKINI SASA
Hata hivyo, ukiachana na ushindi huo wa Kayumba, kuna mambo ambayo yalizua gumzo ukumbini hapo ambapo u-team wa majaji. Wasanii waligawanywa katika makundi ya Madam Ritha, Salama Jabir na Master J na kuonekana wazi hasa pale mshiriki wa jaji mmojawapo alipokuwa akipongezwa tofauti na ilivyokuwa kwa yule ambaye si wa timu yake, jambo lililolalamikiwa na mashabiki.
Mashabiki wengi walisema, siku ya fainali, majaji hao ‘wanaojua kusema’ wangekuwa kimya kama inavyokuwa kwenye shindano la Miss Tanzania.
5
Majaji wakiwa kwenye meza yao ya kuratibia mashindano hayo.
MFANO NI SALAMA
Katika kipengele hicho cha u-team, jaji Salama Jabir alionesha mapenzi yake waziwazi kwa Kayumba baada ya kumsifia kutokana na kupafomu Wimbo wa Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’ katika raundi ya mwisho.
Salama alisema: “Bwana wee gitaa kitu gani? Sisi watu wa uswahilini bwana, tuna mambo yetu na hayo mambo ya gitaa kwanza hatujayazoea, hongera Kayumba.” (akimaanisha kuwa, Nasibu Fonabo hakufanya kitu baada ya kupafomu na gitaa).
MASHABIKI WASEMA KAYUMBA ALIANDALIWA
Baada ya ushindi huo wa Kayumba, gumzo kubwa liliibuka mashabiki ukumbini hapo wakidai kuwa aliandaliwa mapema kutwaa taji hilo kwa msimu huu kwani baadhi ya kura zilionesha mapema.
“Bwana wee, yaani hapa ni kama tumeliwa. Inaonesha kuwa nyuma ya pazia Kayumba aliandaliwa toka kitambo awe mshindi kwani utaona hata majaji wenyewe, kama Salama alionesha wazi mapenzi yake kwa mshiriki huyo,” alisema mmoja wa wahudhuriaji.
8Msanii kutoka nchini Nigeria, Run Town anayetamba na kibao chake cha Gallardo, akipagawisha jukwaani hapo.
KUNA UPENDELEO WA WANAUME?
Katika hatua nyingine, baadhi ya mashabiki walisema mashindano hayo yametawaliwa na uchaguzi wa wanaume tu licha ya muandaaji wake kuwa mwanamke.Walisema mpaka juzi, BSS imetimiza misimu nane huku sita ikitwaliwa na wanaume tu, jambo lililotafsiriwa kuwa huenda waandaaji wake hawazingatii usawa.
9
Mmoja wa washiriki waliokuwa wakichuana jukwaani hapo, Angel Marykato akisaka milioni 50.
KUMBUKUMBU YA WIKIENDA
Ilibidi gazeti hili lifukue kwenye kumbukumbu zake za nyuma na kubaini kwamba, washiriki waliowahi kutwaa taji hilo tangu kuanzishwa mwaka 2006 ni Jumanne Idd (mwanaume), Pascal Casian (mwanaume), Emmanuel Msuya (mwanaume), Misoji Nkwabi (mwanamke), Walter Chilambo (mwanaume), Mariam Ramadhan (mwanamke), Haji Ramadhan (mwanaume) na sasa Kayumba Juma (mwanaume).
11Msanii wa Dansi Christiani Bella akitunza na mashabiki wake wakati akitumbuiza kwenye fainali hizo.
UKUMBI PIA WAZUA MANENO
Baadhi ya mashabiki walisema kutokana na mashindano hayo kuwa makubwa, yangefanyiwa kwenye ukumbi mkubwa zaidi kama ilivyozoeleka kuliko kupeleka sehemu ngeni.
MADAM NA GAUNI LA BEI MBAYA
Lingine lililozua gumzo ukumbini, ni Madam Ritha kuvaa gauni ambalo lilikadiriwa kuuzwa dukani kwa shilingi laki tano.
Ijumaa Wikienda lililazimika kumfuata Madam kwa lengo la kujua bei ambapo alisema alilitungua dukani kwa shilingi milioni moja na laki nane (1,800,000).

NAY WA MITEGO NA LULU:UCHAGUZI UKIISHA ATUTA WAPA TENA SHIKAMOO. KUMBE NDIVYO WALIVYO KWENYE MAJUKWAA.

hii imekuja pale tu wasanii hawa kuona akuna utofauti kati ya mzee na kijana yani yule unaye mweshimu anaweza kuvunja heshima yake kwa ajili ya siasa na kuongea madudu mbele za watu kisha uchaguzi ukipita anaitwa mweshimiwa kweli aina maana. heshima ni wakati wote wa maisha ili ueshimiwe basi onyesha heshima kwanza sasa wanasiasa wetu wamesaau watanzania wanatakiwa kuambiwa nini juu ya maisha yao walichobaki ni kulushiana vijembe tu uku mtanzania mwenye maisha magumu nawewe unashangilia 

HATARE SANA:MSHINDI WA BSS AONGEZEWA SH. MIL 10

1
:Jaji Mkuu wa Mashindano ya Bongo Star Search ‘BSS’, Ritha Poulsen ‘Madam Ritha’, akielezea mipango ya  fainali ya mashindano hayo itakavyokuwa siku ya Ijumaa Oktoba 9 mwaka huu katika Ukumbi wa  King Solomon Hall uliopo eneo la Namanga Kinondoni jijini Dar es Salaam.
2
Mmoja wa washiriki wa shindano hilo, Nassib Fonabo, akiimba kwenye kikao hicho.
3
Angel Kato ambaye ni mshiriki wa shindano hilo, akiimba mbele ya waandishi wa habari.
4
Mshiriki wa shindano hilo, Frida Amani, ‘akichana’ mistari mbele ya waandishi wa habari.
5
Madam Ritha akiwatambulisha washiriki.
SHINDANO la kusaka vipaji vya muziki, Bongo Star Search (BSS) linalotarajiwa kufanyika Oktoba 9, limeongeza  zawadi ya mshindi wa shindano hilo  ambapo sasa atajinyakulia shilingi milioni 60,  ambapo shilingi milioni kumi zitapelekwa studio kwa ajili ya kusaidia shughuli za kurekodi.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari,  Jaji Mkuu wa shindano hilo Ritha Paulsen ‘Madam Ritha’, alisema kuwa shindano hilo lina  msisimuko wa kipekee kwa kuwa washiriki wote ni wazuri kiasi majaji wanapata wakati mgumu kumchagua  mshindi.
“Mshindi wa shindano hili ataondoka na sh. milioni 60, katika kinyang’anyiro cha safari hii chenye  msisimko mkubwa hadi hata sisi wenyewe tunapata wakati mgumu kama majaji,” alisema Ritha
Fainali za shindano hilo zinatarajiwa kufanyika Ijumaa Oktoba 9 Mwaka huu  katika Ukumbi wa King Solomon  uliopo eneo la Namanga Kinondoni jijini Dar es Salaam.  Siku hiyo pia kutakuwa na burudani za nguvu kutoka kwa msanii Run Town wa Nigeria ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Gallardo.
“Ukiachia mbali msanii huyo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa Christian Bella, Yamoto Bendi, Nevy Kenzo ambao watakamua sambamba na wasanii mahiri ambao ni zao la BSS kama Peter Msechu na Kala Jeremiah.  Viingilio siku hiyo vitakuwa 25,000/=, ambapo nafasi za VIP zitakuwa 50,000/= na viti maalum vitalipiwa 100,000/=.  Nawaomba mashabiki waje kwa wingi maana fainali ya mwaka huu ni ya kipekee kabisa,” alisema Madam Ritha.

KATIKA KUTHIBITISHA KUWA MTOTO NI WAKE>>>DIAMOND AMETUPIA PICHA HIZI NA KUSEMA HAYA


TAZAMA PICHA MTOTO TIFFAH PLATNUMZ NI HATAREE



TAZAMA RAY C NA SHEPU YAKE MPYA ATANGAZA KURUDI RASMI KWENYE MUZIKI





FIGURE NDO HABARI YA MJINI:TAZAMA LULU MICHAEL AKIWA ANAPIGA ZOEZI AKITENGENEZA SHEPU



A-Z Kilichotokea Kwenye Party ya Tiffah – Part 1

BONGE LA SOO! Ray KIGOSI Aangua Kilio Ukumbini!

IMG_2017
Msanii wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’ akibembelezwa.
WAANDISHI WETU
BONGE la soo! Katika hali ya kushangaza, msanii wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’ hivi karibuni alijikuta akiangua kilio ukumbini baada ya mshindi wa shindano la kusaka vipaji vya kuigiza kufananishwa na marehemu Steven Kanumba.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta, jijini Dar kulipokuwa na fainali za Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo washiriki 10 ndiyo walikuwa wakiwania kitita cha shilingi milioni 50.
Mara baada ya mshindi wa shindano hilo kutangazwa, ukumbi mzima ulizizima kwa kelele za furaha na kwenda kumpongeza Dennis Laswai aliyeibuka kidedea na wengi walikubaliana kuwa ni haki yake kutokana na kufanya vizuri.
IMG_2026Wakati mshindi na mashabiki wake wakiendelea kufurahia ushindi, kundi la vijana lilipanda jukwaani wakiwa wameshika fulana yenye picha ya marehemu Kanumba huku wakisema mrithi wake amepatikana.
Ndipo ghafla, Ray ambaye alikuwa na upinzani wa kisanii na muigizaji huyo, alipoanza kumwaga machozi hadharani na kujikuta amezungukwa na watu wakimshangaa.
“Jamani mrithi wa Kanumba amepatikana rasmi baada ya miaka mitatu kuishi bila yeye, sasa jembe limerejea tena, mama yetu hapaswi kuwa na simanzi kila siku,” kijana mmoja alisikika akisema huku akienda kumshika mkono mama Kanumba.
Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Ray baada ya mmoja wa vijana hao kumfuata na kumuonesha fulana hiyo ambapo alizidisha kilio kiasi cha wenzake kumfuata na kumtuliza ili awe katika hali ya kawaida.
IMG_2030Mtu mmoja ukumbini hapo alibeza kilio hicho, akisema hiyo yote ilitokana na kuzidisha ‘kiburudisho’ na wala haikuwa kwa sababu ya kummiss sana marehemu kwani hawakuwahi kuwa na ukaribu wa kiwango hicho.
“Ray hana lolote, pale amezidisha kiburudisho tu, hakuwa na mapenzi na Kanumba kiasi hicho mpaka leo hii alie vile, ni usanii tu hakuna lolote. Wapo watu wa kulizwa na kitu kama kile na si yeye, halafu Ray huwa hana ushirikiano mzuri na wasanii wenzie hasa wa kiume,” alisema mtu huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Kwa upande wake Ray alisema kilichomtoa machozi ni ukweli kwamba mshindi ana kipaji cha hali ya juu na yeye binafsi alipenda ushindi wake kiasi kwamba mawazo yake yalimfikisha mbali.
Imeandaliwa na Shani Ramadhani, Mayasa Mariwata na Musa Mateja.

TAZAMA PICHA NA VIDEO ZA MTOTO WA DIAMOND PLATNUMZ

  

WATCH THE VIDEO!!



BUSU LA WEMA, MAKAMBA MH!..NI SHEEDAH-->>

DAH HEBU JIONEE MATUKIO HAYA NDIO UTAJUA KWA NINI WALE WALIOTOSWA NA DIAMOND KAMA MAMAA WA MICHIRIZI WANA WEWESEKA NA LAVIDAVI LA SUKARI YA WAREMBO DUH JAMAA LINA CARE BWANA TAZAMA HUMU ZARI NA TIFFA WANAVYO FAIDI MATUNDA YA CHIBU>



http://www.mambomsetotz.com/2015/08/dah-hebu-jionee-matukio-haya-ndio.html

FRAVIANA MATATA SENDOFF NDANI YA PANDE ZA SHINYANGA

CUSTOMIZED DRESS from scrach….ikiwa imesimamiwa na ze stylist ROSE KOKUHILWA ‘FASHION JUNKII’
Ni kwa neema tuuuuuu na rehemaaa, ni kwa neema tuu……ndo nyimbo ilikuwa inaunguruma kwa spikaaa na mabiharusi na mwenzie akawa wanaingia kwa kunesa nesa

TAZAMA PICHA ZA MAUNO YA MABINTI HAWA

TAZAMA VIDEO MPYA YA SNURA MAJANGA NI FULL MAUNO

TAZAMA PICHA NA VIDEO ZA CHUMBA CHA MTOTO WAKE DIAMOND PLATNUMZ "TIFFAH PLATNUMZ"

INASIKITISHA SANA.!!, SHILOLE AANDIKA UJUMBE MZITO BASATA, KUMBE ANASOMESHA WATOTO YATIMA? SOMA HAPA

1.Kwanini barua imekuja baada ya kupost show yangu ya kwenda Marekani kufanya show?

2.Mmenifungia muziki wangu,Mnataka nikaishi wapi?na mnasema vijana tujiajiri,ajira niliyojiajiri ni hii mnataka nifanye ipi?

3.Nina familia ya watu 10 ndani kwangu,wote wananitegemea wengine wanasoma Boarding,nina watoto yatima wengine wanasoma kupitia muziki huu huu na ninalipa kodi ya nyumba,Mnataka Basata tufanye nini?

4.Ninahangaika,ninapambana na kazi zangu kwa nguvu zangu,Mnataka nikajiuze nipate ukimwi?mnataka nikabebe Dawa za kulevya nikauwawe?kwa sababu najituma kwa kazi yangu na nguvu yangu kama mnavyoona kwenye jukwaa hata vitabu vya Mungu vinasema asiyefanya kazi na asile.
KUTAZAMA PICHA na VIDEO ZAIDI BONY3ZA HAPO CHINI

TAZAMA PICHA WANACHIKIFANYA DIAMOND PLATNUMZ NA ZARI THE BOSS



 

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana