
Muigizaji mwenye mvuto wa aina yake Bongo Movies, Yobnesh Yussuph ‘Batuli’ katika mahaba mazito na mchekeshaji Stan Bakora.
Musa mateja
DAH! Wakati mashabiki wake wakiamini si mtu wa ‘kurukaruka’ kivile, muigizaji mwenye mvuto wa aina yake Bongo Movies, Yobnesh Yussuph ‘Batuli’ amekwaa aibu baada ya picha zake zikimuonesha akiwa kimahaba chumbani na mchekeshaji Stan Bakora kuvuja, Ijumaa linakupa mchapo kamili.

Chanzo kilichovujisha ubuyu huo kilieleza kuwa, kina picha zinazomuonesha Batuli akiwa kimahaba na Stan bila kujua walizipiga kwa ajili gani.
“Nina picha za Batuli akiwa na kanga moja, anaonekana yuko na Stan Bakora ‘on bed’, sijajua wamezipiga za nini ila ukiziona nadhani unaweza kuzifanyia kazi,” kilidai chanzo hicho.

Baada ya picha hizo ambazo kimsingi ziko kinyume kabisa na maadili ya Kitanzania (kwenye filamu haziwezi kuonekana na hata kwenye gazeti haziwezi kuchapishwa) kutua kwenye dawati la gazeti hili, jitihada za kupata undani wake zilianza kwa kuwatafuta wahusika.

Paparazi: Mambo Batuli?
Batuli: Safi vipi kuna usalama huko maana asubuhi sana hii?

Batuli: Mmmh… Tafadhali hizo picha kuna ‘project’ nimefanya na Stan Bakora kwa hiyo naomba zisitumike kunichafua maana mimi kuna ishu muhimu sana natarajia kuifanya kipindi hiki cha uchaguzi.

Batuli: Ujue hizo picha najua atakuwa kakupatia Mkude Simba na lengo lake ni kufanya promo ya muvi yake, mimi sitapenda kwa kipindi hiki nichafuke, please naomba usizitumie.

Batuli: Nimekwambia ni filamu na sitaki zitumike kunichafua.
Paparazi: Hiyo filamu mlishuti wapi?
Batuli: Morogoro ila mimi sikutaka kukaa kambini, nilienda kushuti na kurudi zangu Dar.

Alipotafutwa Stan Bakora kuhusiana na picha hizo na kama ana uhusiano wa kimapenzi na Batuli, alisema:
“Ni muvi kaka, katika hali ya kuuvaa uhalisia ndiyo tulipiga kimahaba zaidi lakini sina uhusiano wowote na Batuli.”
Post a Comment