Featured

    Featured Posts

Diamond, Kajala Mahaba Niue!

Diamond, Kajala Mahaba Niue!
NI gumzo! Ubuyu motomoto ambao unasambaa kwa kasi ya ajabu kama moto wa kifuu mjini unadai kuwa,  staa nambari moja Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwigizaji Kajala Masanja wamedaiwa kuwa ni wapenzi na sasa ni mahaba niue, Risasi Jumamosi limesheheni full stori.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, uhusiano wa Diamond na Kajala  unadaiwa kuibuka ghafla miezi kadhaa iliyopita lakini wamekuwa wakifanya siri nzito kabla ya hivi karibuni kukolea zaidi baada ya mpenzi wa Diamond, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kurudi nchini mwake, Afrika Kusini ‘Sauz’.
“Walianza zile za kimjinimjini, wakawa wanafanya yao kimyakimya tangu Zari akiwepo lakini mahaba niue yamekuja kushamiri zaidi baada ya Zari kutimkia zake Sauz,” kilisema chanzo chetu.
MASTAA WAZUNGUMZIA
Mara baada ya chanzo hicho kumwaga ubuyu huo, Risasi Jumamosi lilipenyezewa data kutoka kwa mastaa tofauti ambao wanafahamu uhusiano huo mpya ambao pia ulianza kusambaa taratibu katika mitandao ya kijamii.
“Hivi kwani nyinyi hamjaipata habari hii? Diamond amemnasa Kajala na mambo yao ni bambam. Sema kiukweli Diamond ni msiri maana unajua ana mambo mengi hivyo hapendi kabisa hii ishu ijulikane,” alisema staa mmoja mkubwa Bongo huku akiomba hifadhi ya jina.
Kama hiyo haitoshi, staa mwingine aliliambia Risasi Jumamosi kuwa, dada wa Diamond, Esma anaujua mchezo mzima na anatajwa kuusambaza ubuyu huo kama malipo kwa Wema (Sepetu) anayemtuhumu kumuibia bwana wake, Petit Man.
“Esma ameamua kumwaga ugali maana Wema na timu yake wamekuwa wakijitapa sana mjini kwamba wamemnyakua mume wa Esma, Petit Man. Na yeye anawaonesha kwamba kama ni kuchukuliwa mbona hata Kajala amechukuliwa na Diamond ambaye alikuwa mtu wa Wema lakini wamekaa kimya,” alisema msanii huyo.
Jitihada za kumpata Esma ili aweze kuzungumzia suala hilo ziligonga mwamba baada ya simu yake ya mkononi kuita muda mrefu bila kupokelewa.
MITANDAO YAZIDI KUKUZA JAMBO
Mpaka tunakwenda mitamboni, juzi, mitandao mbalimbali hususan Instagram, wadau walisambaza habari ya Kajala na Diamond huku wakijaribu kumwambia Zari amtambue Kajala kama mke mwenzie kwani ameshalala Madale, nyumbani kwa Diamond.
“Zari mke mwenzio ni huyu hapa, anakusaidia. Juzi amelala Madale na Diamond,” iliandikwa na mdau mmoja wa Instangram.
ZARI ACHANGANYIKIWA
Chanzo kilichomwaga ubuyu huo kimeeleza kuwa, taarifa za Kajala na Diamond zilipomfikia Zari, alichanganyikiwa na kuanza kumcharukia Diamond au baba Tiffah ambaye ilibidi atumie nguvu ya ziada kumtuliza kwani bado wawili hao wanaendeleza uhusiano wao huku wakijua Zari hayupo Bongo.
“Zari alicharuka kwelikweli. Ilibidi Diamond atumie nguvu ya ziada kumtuliza na bahati nzuri mtoto wa kike ameelewa,” kilisema chanzo chetu.
DIAMOND SASA
Alipotafutwa Diamond na kusomewa mashitaka yake, mambo yalikuwa hivi:
Risasi Jumamosi: Kuna taarifa kwamba unatembea na Kajala na sasa mahaba ni motomoto, vipi kuna ukweli? Tena vyanzo vingine vinadai kuna hadi picha za wewe na Kajala mkiwa nyumbani kwako, unazungumziaje hilo?
Diamond: Aaah! Siyo kweli mwanangu…picha kweli mnazo? Picha gani…yaani kiaje?
Risasi Jumamosi: Inasemekana zipo ambazo mpo nyumbani kwako, Madale.
Diamond: Aahaha! Aaah uongo mtupu siyo kweli. Kama kuna picha kweli nitumieni basi.
KAJALA SASA
Alipopigiwa simu zaidi ya mara tano, Kajala hakupokea. Risasi Jumamosi lilimtumia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) uliosomeka hivi:
“Habari, kuna ishu yako hapa Global Publishers, inahusu madai ya wewe kutoka kimapenzi na Diamond jambo ambalo linadaiwa kuleta mtafaruku mkubwa kati yako na Zari. Pia hata kwenye mitandao ya kijamii bila shaka umesikia, naomba ufafanuzi wako tafadhari.”
Licha ya ujumbe huo kuonesha kumfikia, hadi tunakwenda mitamboni, Kajala hakujibu chochote.
KAMA NI HIVYO
Madai ya kuwepo kwa uhusiano huo yanaweza kumweka Kajala katika mtazamo mwingine kijamii, kwani miaka miwili nyuma alidaiwa kutoka kimapenzi na mwanaume anayeitwa CK ambaye hakuna shaka alikuwa mpenzi wa Wema kabla ya kumwagana.
Hali hiyo ilizua mjadala, Kajala alibebeshwa madai mazito kwamba alikuwa na uhusiano na CK hata akiwa na Wema, ikitafsiriwa kwamba alikuwa akimlia vyake mwenzake hali iliyozua mgogoro wa wawili hao.
Diamond naye, amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema, wakamwagana. Kitendo cha kudaiwa kutoka na Kajala, kinazidi kumweka mdada huyo katika mlolongo wa kudhaniwa anamwandama Wema kwa vile kila alikopita, yeye naye anapita!
Chanzo: GPL

FAHAMU HII NDO ROHO YA WEMA SEPETY KWA SASA




 During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip

Flora Mbasha akiri: Mwanangu si wa Mbasha!

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha na aliyekuwa mumewe, Emmanuel Mbasha.
Waandishi wetu
OHOOO! Kimenuka tena. Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amesema mwanaye mdogo (jina linahifadhiwa) hahusiani hata kidogo na aliyekuwa mumewe, Emmanuel Mbasha huku akidai kuwa anamtambua mwanaume huyo kama mzazi mwenzake kwa mtoto mmoja tu (Liz), Risasi Jumatano linakupa zaidi.
Akizungumza na waandishi wetu kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki, Flora alisema amechoshwa na manenomaneno yanayosemwa juu yake na Emmanuel na kwamba kama mumewe huyo ameamua kumwaga ugali, yeye yupo tayari kumwaga mboga.
Mwimbaji huyo alisema kwamba kauli aliyoitoa hivi karibuni kuwa anampenda mumewe na kwamba yupo tayari kuishi naye haikutoka moyoni, isipokuwa alifanya hivyo kwa huruma tu, kwa sababu mwanaume huyo ni mtu katili, mwenye roho mbaya na asiyemuogopa Mungu.
“Mtu mwenyewe alimtelekeza mtoto (Liz) kwa zaidi ya mwaka mmoja, ni mtu mbaya sana, sina mapenzi na Mbasha hata kidogo, ni afadhali niolewe na chizi anayeokota makopo kuliko kurudiana na mtu katili na mnyama kama huyo, namheshimu kama mzazi mwenzangu kwa Liz,” alisema.
Mtoto anayedaiwa kuibua mazito.
“Huyo mwanaume hafai kabisa, ni katili, namfananisha na shetani, anajifanya mwema kwa watu wakati hajawahi kuiomba msamaha familia, sikubaliani kabisa na hukumu ya mahakama, ukweli anaujua kwamba alibaka na hata mkimtaka huyo binti mumhoji nitamleta, isitoshe sasa hivi hata mtoto wake hamjali, hajui anasoma vipi, hajawahi kulipa hata shilingi ya ada, mimi mwenyewe ndo nahangaika kumlea mwanangu Liz ambaye anasoma kidato cha kwanza.
“Hastahili kabisa kuitwa baba sababu mzazi mwenye akili hawezi kutelekeza familia hata kama tumegombana, nimemwachia nyumba niliyojenga kwa pesa yangu na pesa zote aliweka kwenye akaunti yake na zote nilimwachia lakini kashindwa kuihudumia familia.”
Flora anajulikana kuwa na watoto wawili, mdogo akiwa ni yule aliyezaliwa wakati wanandoa hao wakiwa katika mzozo uliosababisha watengane hadi hivi sasa. Alipoulizwa kwa nini anadai aliyekuwa mumewe kumtelekeza mtoto mmoja tu, badala ya wawili, alifunguka.
“Huyu mwanangu mdogo hausiki naye kabisa, tena asiwe anamtaja kabisa kwa sababu hamhusu, hajui hata matumizi yake yakoje, mengine kaka achana nayo tu,” alisema Flora.
Mwimbaji huyo mwenye kipaji alipoulizwa sababu za kufuta kesi ya kudai talaka, aliyoifungua hivi karibuni katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati anadai hamtaki na hawezi kurudiana naye, alisema alifanya hivyo baada ya kushinikizwa na mtu ambaye hata hivyo, alikataa kumtaja.
Mwimba Injili Bongo, Flora Mbasha.
Flora alisema familia yake haijaridhishwa kabisa na suala la kesi ya ubakaji iliyokuwa ikimkabili mumewe kumalizika kwa kuachiwa huru na kwamba wanajipanga kwa ajili ya kukata rufaa.“Hiyo kesi imeisha kisiasa, Mbasha aliwahi kukiri kuwa ni kweli alifanya kitendo hicho, iweje leo aonekane hana hatia? Tutakwenda kukata rufaa ili haki itendeke.”
Baada ya kuzungumza na Flora, mwandishi wetu alimtafuta Mbasha kwa lengo la kumuuliza kuhusu madai ya mtoto yule mdogo kutohusika naye kama alivyosema mkewe, naye bila ‘kutafuna maneno’, alisema hata yeye hamtambui huyo mtoto mdogo, ila anaomba arudishiwe mtoto wake mkubwa, Liz na maisha mengine yaendelee.
“Hata mimi simtambui huyo mwingine, ninachoomba anirudishie tu mtoto wangu mkubwa Liz, huyo mwingine sihusiki naye kabisa kama alivyosema, yeye (Flora) ndiye anajua mhusika wa huyo mtoto, lakini si mimi na wala hajakosea kusema hivyo, nililitambua hilo tangu zamani, anipe tu mwanangu wa kwanza,” alisema Mbasha.
Imeandikwa na Brighton Masalu, Mayasa Mariwata na Gladness Mallya

SHILOLE NA NUH MZIWANDA SASA WAAMUA KUJIACHIA KWA STYLE HII..



TAZAMA PICHA MATATA ZA KAJALA MASANJA....LAZMA UDENDA UKUTOKE



http://www.mambomsetotz.com/2015/08/hii-ndiyo-siku-ambayo-kajala-alivaa.html

BAADA YA DK CHENI KUTANGAZA NDOA, MAMA LULU AMPA BINTIYE RUKSA KUOLEWA KIISLAM!

Staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa na mamaake.
MAGEUZI! Mama mzazi wa staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila ametoa baraka kwa bintiye huyo ambaye kiimani ni Mkristo, kufunga ndoa ya Kiislam kwa madai kuwa ndoa si dini bali ni utu wa mtu. 
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kuna barua za posa mbili ambazo mwanamke huyo mwenye misimamo amekuwa akizikataa kutokana na wahusika kuwa na imani tofauti na Lulu.CHANZO CHAANIKA MSIMAMO WA MAMA LULU

“Unajua mama Lulu ni mwanamke mwenye misimamo sana. Akishikilia jambo kashikilia. Posa mbili zilishafika akagoma katakata, kisa waoaji si Wakrsito. Lakini hilo nalo limeonekana kumuumiza kisaikolojia Lulu maana hajui ni mwanaume gani aliyepangiwa na Mungu.


“Watu wengi wamekuwa wakimlaumu sana mama Lulu wakidai kuwa anakataa posa za wanaume wa Kiislam kwa kigezo cha dini lakini kumbe anataka tu akae na mwanaye pale nyumbani.”

“Ninavyojua mimi, kikubwa kilichokuwa kikimfanya mwanamke huyo ashikilie msimamo huo ni historia yake. Anasema katika ukoo wake na wa baba Lulu (Michael Kimemeta) hakuna Muislam (mwanaume) aliyeoa hapo wala Mkristo (mwanamke) aliyekwenda kuolewa na Muislam,” kilisema chanzo.



...Baba Lulu.

MAHOJIANO

Amani lilimuuliza kama miongoni mwa wachumba wawili waliojitokeza kumchumbia Lulu wakakataliwa, yupo staa wa sinema za Bongo, Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ ambaye hivi karibuni aliripotiwa na gazeti ndugu na hili (Ijumaa) kuwa siku hizi yupo ‘vere klozdi’ na Lulu, mahaba yakatajwa, lakini alitoa majibu ya njia panda bila kusema ni kweli au kinyume chake!

Chanzo: “Sina hakika. Ila wapo wawili. Nadhani mama Lulu mwenyewe anajua. Nendeni mkazungumze naye. Ila ni mtata sana yule mama, si wa kumwingia kirahisirahisi tu.”

Amani: “Kwani Lulu mwenyewe alikuwa tayari kuolewa Kiislam?”
Chanzo: “Inasemekana yeye yuko tayari.”


KUHUSU BABA LULU

Amani lilimuuliza mtoa habari huyo kama anajua msimamo wa baba Lulu kuhusu mwanaye kubadili au kutobadili imani.Chanzo: “Unajua yule mzee ana maisha yake kwa sasa. Ana familia yake. Lulu ni mwanaye lakini naamini mwongozo mkubwa anaupata huku Dar kwa mzazi mwenzake (mama Lulu).”



Dk. Cheni.

MAMA LULU ASAKWA

Juzi, Amani lilimsaka mama’ke Lulu na kufanikiwa kumpata kwa njia ya simu ambapo mahojiano yake na paparazi wetu yalikuwa kama ifuatavyo:
“Labda niseme kwanza mimi mtoto wangu hajawahi kuletewa posa nyumbani, isitoshe hata yeye mwenyewe hajawahi kuniletea mchumba na kuniambia kuwa anataka kumuoa.


“Awali nilipenda mtoto wangu aolewe na mtu wa imani yake kwa sababu yeye mwenyewe amekulia katika Ukristo mpaka kufikia hapa alipo sasa.“Lakini siku hizi wazazi wanaangalia utu wa mtu na vitu vingine vinakuja baadaye kabisa, kwa vile anaweza hata akaolewa na mwanaume wa dini yake bado akamletea shida maishani.

“Ngoja nikwambie, kwanza sidhani kama sasa hivi mapenzi yanaangalia dini wala kabila. Kama yeye atamleta Muislam na kampenda kutoka kwenye moyo wake na mimi nitampokea wala sitakuwa na pingamizi lolote.


AMANI LARUDI KWA DK. CHENI

Baada ya Amani kumalizana na mama Lulu, lilirudi kwa Dk. Cheni anayetajwa hivi karibuni ‘kutoka’ na Lulu ambapo aliulizwa kwa staili kuwa, wasomaji wa gazeti hili wanataka kujua kama kweli atamuoa Lulu. Alijibu:

“Swala la kutomuoa au kumuoa Lulu ni langu binafsi. Hebu subirini msiwe na haraka mtakuja kuujua ukweli. Mbona Watanzania mlio wachache mnakosa uvumilivu? Yaani mnapenda kujua mambo ya mbele kabla wakati haujafika.
“Hebu kaeni chini mtafakari nchi ya Japan wanatengeneza magari lakini nyie hata baiskeli hamuwezi. Tafakarini ubunifu wenu siyo mambo ya watu.”


Amani lilimkosa Lulu hewani lakini maelezo ya mama yake kama mkuu wa familia yalitoa picha ya msimamo kuhusu binti huyo ambaye hivi karibuni aliripotiwa kujikita kwenye maombi kwa kusali na kumwabudu Mungu katika roho na kweli japo mara kadhaa amewahi kunaswa akipombeka kama ishara ya shetani kumzidi mabavu.

MWALIMU WENU NAWATOBOLEA SIRI KIDOGO YA DIAMOND NA ZARI.... HATIMAYE MTOTO WA KIGANDA ASEMA UKWELI...TAZAMA HAPO CHINI

Hii picha ni ya jana ijumaa ila haikueleweka kama walikuwa wametoka msikitini au ni mavazi ya swaggz ila ni katika mitoko yako ya weekend hii usije kushtuka utakapokutana na couple fulani ya ‘Ameizing’ ya TZ+UG, sababu Zari Tlale a.k.a The Boss Lady yupo ndani ya jiji la Dar au kama anavyopaita mrembo huyo D-City.  


 D-city1
Kupitia Instagram mrembo huyo wa Uganda ambaye makazi yake yako Afrika Kusini amepost picha kadhaa akiwa na mpenzi wake Diamond Platnumz kwenye Gari aina ya BMW
d-city3Licha ya sasa kuwa Diamond na Zari wanajulikana kuwa nai wapenzi lakini wanapoulizwa juu ya Uhusiano wao wamekuwa wakikanusha na kusisitiza kuwa wanaproject ya pamoja.Lakini safari hii amethibitisha mwenyewe kwa kauli yake baada ya kumuita Girlfriend wa dancer wa Diamond 'wifi'

zari d-city

KESI YA FLORAH MBASHA AKIDAI TALAKA YASIKILIZWA TENA...FATILIA HAPA


October 6 2015 waimbaji wa gospel ambao ni wanandoa, Flora Mbasha na mumewe Emmanuel Mbasha walifika Mahakamani kwenye kesi ya madai ya talaka iliyofunguliwa na Flora,Bofya Video hapo chini umsikie Florah alichoamua baada ya kufika Mahakamani Tar Tajwa Hapo Juu.

IRENE UWOYA MBUNGE MTARAJIWA AKIWA NDANI YA VAZI LA KANGA

TAZAMA PICHA SEKI WA ZE KOMEDY ORIGINAL AKIWA ANAFUNGA NDOA

HIRIZI YA MTOTO TIFFAH YAZUA GUMZO KWA LULU MICHAEL


BOND NA WASTARA MAMBO SAFI......TAZAMA WAKILANA NDIMI

Ikiwa Bado Kuna Sinto fahamu Kwa Mashabiki wa Filamu Kama Bond na Wastara ni Wapenzi kweli ama la , Mwigizaji na Mtangazaji Bond Ameandika Maneno Haya na Kupost Picha hiyo Hapo juu Kwenye Ukurasa Wake wa Facebook:

"Siku ya Tarehe 27 mwezi wa 9 mwaka 1994 ni siku Mama yangu alinifariki na kuniacha mpweke na nikajiona kuwa sitakuwa na furaha.
Lakini tarehe hiyo hiyo 27/09 kasoro mwaka alizaliwa binti mmoja mzuri wa ajabu mwenye sifa nyingi nzuri ambazo kila mtanzania anazijua kuanzia kazi, upendo, huruma, uvumilivu na ujasiri kwakweli mungu hajawahi kukosea wala hatokosea kufanya maamuzi
Kwani humpa amtakae na humnyima amtakae na yote ikiwa ni kwa kheri zake
Asante mungu kwa kunijaalia kunipa na kumjua huyu mwanamke mzuri"

TAZAMA JACK WOLPER AKIWA KATIKA POZI ZA KIMAHABA NA MPENZI WAKE




MAHABA NIUE: TAZAMA MAPENZI YA ALIKIBA NA JOKATE "KIDOTI" YALIKOFIKIA

UZEE KWELI MWISHO CHALINZE:TAZAMA MAMA DIAMOND PLATNUMZ AKIWA ANAOGA

TAZAMA PICHA ZARI THE BOSS LADY AKIWA NA WANAWE WANNE



RAY: Heshimuni Maamuzi Yangu ya Siasa...Nyinyi Tukaneni Mpaka Mchoke Maana Hata Mkwaruzo Sijapata

(  FREEDOM OF SPEECH )
Nyinyi tukaneni mpaka mchoke maana tangia muanze kutukana matusi hata mkwaruzo sijapata msinilazimishe kupenda mnachokipenda nyinyi. Heshimuni maamuzi yangu kwani kila mtu ana haki ya kufanya maamuzi anayoyaona kwa upande wake ni sahihi, nasema hivi wananchi wana akili timamu hawawezi kuwapa ridhaa ya kuongoza nchi hii kama wenyewe kwa wenyewe mnagombana mtaweza ongoza nchi hii mnavyoona watu wanajaa kwenye mikutano yenu mnafikiri mnapendwa hao wamekuja kuwashangaa mawaziri wakuu wawili waliohama chama tawala alafu kabila moja nasemaje kama umeshindwa kuiongoza familia yako utaiweza ya mwenzako amuwezi pata madaraka ya nchi. komaeni kwanza kisiasa labda miaka amsini ijayo ndio tuwafikirie kuwapa nchi baada ya kujiridhisha kama mshakomaa kisiasa. Over....Ray

DIAMOND PLATNUMZ KUNYANG'ANYWA MTOTO....FATILIA KISA HAPA

Musa mateja
Kazi ipo! ‘Kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, amekumbwa na hofu ya kunyang’anywa mwanaye anayemuita malkia, Latifah Nasibu ‘Princes Tiffah’ baada ya mama mtoto wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kutimka naye kwenda kwao nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.

Latifah Nasibu ‘Princes Tiffah’.
Habari kutoka ndani ya familia ya staa huyo zilieleza kwamba, wikiendi iliyopita Diamond alisikika akiwaambia jamaa zake kuwa ana hofu hiyo na kwamba haamini kabisa kuondoka kwa Zari na Tiffah kwani anahisi huko aliko maadui zake wanaweza kumteka mwanaye kwa kuwa siku zote wamekuwa wakiongea maneno machafu.
“Alikuwa amekaa na washikaji zake na mimi nilikuwepo, alikuwa anatia huruma kweli maana tulikuwa tukipiga stori mara ghafla nikamuona amechenji baada ya kumuuliza akaniambia anamuwazia sana mwanaye Tiffah huko South kwani anahisi uwepo wake kule anaweza kutekwa na kujikuta akifanyiwa mambo yasiyokuwa sawa na baadhi ya wabaya wake ambao wamekuwa wakimuombea mabaya kila kukicha.
“Diamond anasema hana amani sana kwani amekuwa akimuomba Zari asiende hadi mtoto afikishe angalau miezi tisa lakini amegoma kufuatia miradi yake kuyumba kwani amekuwa mbali nayo kwa muda mrefu.

‘Kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
“Unajua Zari amekaa miezi mingi sana tangu alipotimba Bongo kujifungua, ungekuwa uwezo wake na si sheria za nchi angefanya kila liwezekanalo amhamishie huku maana hafurahishwi na kitendo cha kuwa mbali na mwanaye Tiffa,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Unajua Ivan (aliyekuwa mume wa Zari aliyezaa naye watoto watatu wa kiume) huwa anakwenda kwa Zari na yule shwahiba wake, King Lawrence ‘so’ lolote laweza kutokea kwani mara kwa mara walishasema kuwa Tiffah ni damu yao hadi wakataka akapimwe DNA.”
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Diamond alikiri kupatwa na hofu hiyo kwani hana imani sana na jamaa hao.
“Mimi kama binadamu lazima niwe na hofu na mwanangu hasa linapokuja suala la kuwa mbali na mimi na ndiye mtoto wangu wa kwanza hivyo lazima niwaze,” alifunguka Diamond.
 

TAZAMA PICHA MTOTO WA DIAMOND PLATNUMZ TIFFAH ALIVYPOKELEWA NA KAKA ZAKE



Watoto wa kiume wa mpenzi wa Diamond Platnumz ‘Zari’ wamempokea mdogo wao Tiffah kwa furaha sana alivyowasili nyumbani kwao nchini Africa Kusini.
Kwenye picha alizopost Zari zimeambatana na ujumbe huu ” If anybody ever said perfect doesnt exist, they were wrong, it surely does, look at my Perfect Lil Life “
zari 00 zari 0 Zari 1 Zari 2 zari 3 Zari 4 zari

TAZAMA PICHA MTOTO WA DIAMOND PLATNUMZ TIFFAH ALIVYPOKELEWA NA KAKA ZAKE


Watoto wa kiume wa mpenzi wa Diamond Platnumz ‘Zari’ wamempokea mdogo wao Tiffah kwa furaha sana alivyowasili nyumbani kwao nchini Africa Kusini.
Kwenye picha alizopost Zari zimeambatana na ujumbe huu ” If anybody ever said perfect doesnt exist, they were wrong, it surely does, look at my Perfect Lil Life “
zari 00 zari 0 Zari 1 Zari 2 zari 3 Zari 4 zari

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana