Orodha ya wachezaji watatu waliongia kwenye fainali ya kuwania tuzo
ya Ballon’Dor inayotolewa kwa mchezaji bora wa dunia imetajwa hii leo .
Orodha hiyo imewajumuisha wachezaji watatu ambao ni nahodha wa timu
ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo , nahodha wa timu ya taifa ya
Argentina Lionel Messi, na Kipa wa timu ya taifa ya Ujerumani Manuel
Neuer.
Ronaldo ndio mchezaji bora kwa sasa baada ya kutwaa tuzo hiyo mwaka
jana.Mchezaji ambaye anatetea tuzo hii hadi sasa ni Cristaino Ronaldo
ambaye aliitwaa kwa mwaka 2013 na kwa jinsi mambo yanavyokwenda ana
nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo mwakani .
Lionel Messi aliwahi kutwaa tuzo nne mfululizo za Ballon’Dor.
Mshindi wa tuzo hii atatangazwa kwenye hafla itakayofanyika huko Zurich januari 12 ambapo tuzo mbalimbali zitatolewa .
Kipa wa Ujerumani Manuel Neur atawania tuzo hiyo dhidi ya Lionel Messi na Cristaino Ronaldo.
Post a Comment