Featured

    Featured Posts

KILICHOTOKEA JANA KUHUSIANA NA HABARI ZILIZO IHUSU BENKI YA NBC


Nianze kuliandikia hili kwa kuonyesha furaha yangu kuwa huwenda sasa kumekua na uelewa juu ya maswala ya usalama mitandao. Nalisema hili kutokana na uhalisia kwamba Jana nilipata maswali kutoka kwa watu wengi sana huku nikipata jumbe nyingi zilizofanana zikielezea juu ya tukio la benk ya NBC kuingiliwa na wadukuzi.

Wengi walinitaka pia nielezee huku nikiulizwa mbona hakuna nilichozungumza. Nilifarijika sana kwani muda uliopita wengi hawakua wakihoji juu ya maswala ya udukuzi pamoja na usalama mitandao na huwenda hii ilitokana na kutokua na uelewa wa maswala husika.

NINI HASA KILITOKEA?

Kwanza kabisa Kulikua na Itlafu ya Umeme ambayo ilisababisha baadhi ya Mashine kuzima.

Pili, Kulitokea Tahadhari ya Moto iliyosababisha wafanyakazi kuchuukua tahadhari ya kutoka nje.

Na Tatu, Mifumo ya Mobile banking (Inayotoa huduma za miamala kupitia simu za kiganjani) kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo iliyo sababisha kutoa kiwango kisicho sawa kwa waliokua wakiangalia salio.

Matukio haya matatu yaliunganishwa na kutengeneza taarifa moja iliyo sambazwa kua kuna mdukuzi aliingilia banki ya NBC na kusababisha mifumo kutofanya kazi na hatimae kuhamisha kiasi kikubwa  cha pesa. Kitu ambapo kilipelekea wafanya kazi kutoka nje ili uchunguzi zaidi uweze kufanywa.

Na anaepata taarifa anapo angalia salio anaona kunatatizo katika kiasi chake na kuamini jumbe ile. Panapotoka ufafanuzi wa taarifa hii wengi bado wanahoji bado kuna shaka niendelee kutoa ufafanuzi nini hasa kinaweza kikawa kimesababisha?



author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana