Katika pita pita zake kamera zimemnasa kijana ambaye hakujulikana jina lake mara moja akiwa amevua nguo zote na kubaki kama alivyozaliwa na kung'ang'ania kwenye daraja la Kidau(Ibinzamata) mjini Shinyanga barabara ya Mwanza Shinyanga. Mashuhuda wanasema kijana huyo kafika darajani leo asubuhi na kuanza kuvua nguo moja baada ya nyingine huku wakisema kuwa huenda amepandisha majini,ama katumia madawa ya kulevya yaliyomchanganya akili
Kijana akikatisha barabarani kwenda upande wa pili wa daraja
Kijana akining'inia darajani,hatukuweza kujua nini kimemsibu kijana huyo
Baadaye aliamua kutoka darajani kisha kuanza kukimbia hivyo barabarani kisha kulala barabarani
Akiwa amesemama barabarani. Mpaka tunaondoka eneo la tukio wasamaria wema walijitokeza kumkamata kisha kumvalisha nguo baada ya tukio hilo.
Post a Comment