Baada ya hivi karibuni kunaswa chobingo
akiwa na mwanamuziki Haroun Kahena ‘Inspector Haroun’, mwanadada
asiyekaukiwa na vituko Baby Joseph Madaha juzikati alibambwa tena
akichezewa kimahaba na njemba ndani ya gari kiasi cha kuwafanya wadau
kuhoji, yeye ni cha wote?.
Baby Joseph Madaha akichepuka na njemba.
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika Pub moja iliyopo Kijitonyama
jijini Dar ambapo mastaa kibao hukutana na kuponda raha. Awali, Baby
Madaha alionekana akiwa anapiga ulabu huku akichezea simu yake lakini
baada ya muda alinyanyuka na kuelekea kwenye gari iliyokuwa imepaki
gizani, ndani kukiwa na mwanaume.
Baada ya paparazi wetu kuusoma mchezo,
alilifuata gari hilo na kuwakuta wawili hao wakifanya yao na ndipo zoezi
la kuwafotoa lilipoanza.
Baby Madaha akikurupuka kuzikimbia kamera za Global.
Wakati paparazi akitekeleza jukumu lake, Baby Madaha alianza
kubwatuka na kutaka asipigwe picha huku akikimbia kuelekea nyuma ya pub
waliyokuwa wakinywa.
Hata hivyo, baada ya Madaha kukimbia paparazi wetu alimfuatilia mwanaume aliyekuwa na mrembo huyo na kugundua kuwa alikuwa ni msanii wa Bongo Fleva anayefahamika kwa jina la Pasha.
Hata hivyo, baada ya Madaha kukimbia paparazi wetu alimfuatilia mwanaume aliyekuwa na mrembo huyo na kugundua kuwa alikuwa ni msanii wa Bongo Fleva anayefahamika kwa jina la Pasha.
Post a Comment