Msanii wa muziki ambaye ni dada wa Nasibu Abdul ‘Diamond’ Mwajuma Abdul ’Queen Darleen’ juzi alikoswakoswa na ajali alipokuwa kwenye msafara wa kumpokea kaka yake aliyekuwa akitoa nchini Afrika Kusini alikozoa tuzo tatu za Channel O Music Video Awards (CHOMVA).
Msanii wa muziki ambaye ni dada wa Nasibu Abdul ‘Diamond’ Mwajuma Abdul ’Queen Darleen’.
Akiwa kwenye msafara huo ulioanzia
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere huku akiwa amedandia
kwenye gari ndogo akiwa ametoa nje sehemu kubwa ya mwili wake, msafara
ukiwa maeneo ya Tazara ghafla lilitokea gari likiwa kwenye mwendo wa
kasi ambalo lilitaka kumzoa lakini dereva akafanya jitihada za kumkwepa.
Hata hivyo, licha ya kukoswakoswa na
ajali hiyo, Queen Darleen alionekana kuendelea kushangilia kana kwamba
hakukuwa na lolote baya lililotaka kumkumba.Msafara wa mapokezi ya
Diamond uliokuwa na watu wengi ulianzia uwanja wa ndege hadi nyumbani
kwake Sinza.
Post a Comment