Upangaji
wa makundi ya timu kumi na sita zilizofuzu kucheza fainali za
mashindano ya 30 ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2015
yamefanyika katika mji mkuu wa Equatorial Guinea, Malabo.
Mashindano
hayo yataanza Januari 17, 2015.Upangaji wa makundi ulirudishwa wiki
moja nyuma ili kuiwezesha Equatorial Guinea, kujiandaa baada ya kuchukua
nafasi ya Morocco, iliyokuwa iandae mashindano hayo, lakini ilishindwa
kufanya hivyo baada ya kutaka mashindano hayo yasogezwe mbele kuhofia
ugonjwa wa Ebola ambao umeyakumba baadhi ya mataifa ya Afrika Magharibi,
ambako zinatoka timu nyingi zinazoshiriki michuano hiyo.
Mabingwa
watetezi Nigeria ni moja ya timu kubwa zilizoshindwa kufuzu kucheza
fainali za mwakani, pamoja na Misri na Angola ambazo zote kwa mshangao
hazitaweza kushiriki.
Haya hapa makundi manne ya AFCON 2015:
Kundi A Equatorial Guinea, Burkina Faso, Gabon, Congo
Kundi B Zambia, Tunisia, Cape Verde, DR Congo
Kundi C Ghana, Algeria, South Africa, Senegal
Kundi D Ivory Coast, Mali, Cameroon, Guinea
Wenyeji
Equatorial Guinea na Congo zitacheza mechi ya ufunguzi wa michuano
hiyo. Kundi D ndilo linaloonekana kuwa gumu zaidi kutokana na timu
zilizopangwa kundi hilo.
Post a Comment