Featured

    Featured Posts

ORODHA YA MASTAA WA KIKE WANAOONGOZA KUIGIZA PESA NYINGI KWA MWAKA HUU

Screen Shot 2014-11-07 at 5.58.04 PMKama hufahamu ni kwamba list ya mastaa wa kike watano wanaofanya muziki walioongoza kwa kuingiza mkwanja mkubwa kwa kipindi cha mwaka 2013-14 nchini Marekani kutokana na kazi zao mbalimbali kama shows na mauzo mengine imetoka.
Beyonce II
No.1- Beyonce: Mauzo ya Albam yake aliyoitoa kwa kushtukiza mwaka 2013, mkwanja alioukusanya katika show zake unakadiriwa kuwa dola bil. 2.4 kwa show ya jiji moja na hesabu zimeonyesha ameingiza jumla ya dola milioni 115 na kuwa mwimbaji aliyezalisha pesa nyingi zaidi kwa mwaka 2014.
Taylor-Swift-Pictures-9
No.2- Taylor Swift: Huyu ni msanii wa kike pekee ambaye mauzo yake yanaweza kugonga platinum kwa mwaka huu huku akikusanya na pato lake kwenye mfuko kwa kutangaza bidhaa, anakuwa na jumla ya dola milioni 64 mwaka huu.
pink-cover-use-only-650
No. 3- Pink: Huenda asiwe mmoja kati ya maarufu waliotawala mainstream kwa sasa lakini pesa aliyoikusanya inafikia dola milioni 52 kupitia show zaidi ya 85 ambazo zimemuingizia kama dola mil. 1 kwa kila show na kitita kingine safi akijipatia kupitia madili yake ya matangazo ya bidhaa.
rihanna
No. 4- Rihanna: Dada lao amekunja mkoba wa kushiba kupitia madili anayofanya na makampuni mbalimbali ya fashion pamoja na kitita alichokikusanya kwenye tour aliyofanya na Eminem, mwaka huu hajaingiza albam sokoni hivyo inaonyesha pia bila kuimba muziki bado Rihanna anaweza kuzalisha pesa nyingi kutoka upande mwingine.
Katy Perry
No. 5- Katy Perry: mkali wa rekodi ya “Dark Horse”, mauzo ya tiketi za show zake sehemu mbalimbali duniani na mkwanja wa deal za matangazo umemfanya akusanye jumla ya kiasi cha dola mil. 40.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana