Featured

    Featured Posts

LIST MPYA,YA 10 BORA YA WATU MATAJIRI NCHINI TANZANIA

Said Salim Awadh Bakhresa.
KATI ya miaka ya 1960 hadi 1980, mtu kuwa tajiri
alionekana ni hatari kwa taifa, tena mali zake alizimiliki
kwa kificho, vinginevyo angeitwa mhujumu uchumi. Lakini
kwa sasa mambo yamebadilika, taratibu sera za kibepari
zinatawala, ujamaa unapewa kisogo.
Mtu kama ni mbunifu, ana nidhamu ya kutofuja pesa na
anafanya kazi sana kwa nini asiwe tajiri? Utandawazi
unasaidia ndiyo maana leo tunaweza kuwatambua
mabilionea wakubwa ambao wanastahili pongezi kwa hatua
walizopiga. Tusisahau kuwa wanaibeba nchi kwa ulipaji
kodi.
1. SAID BAKHRESA
Jina lake kamili ni Said Salim Awadh Bakhresa. Jarida la
Forbes mwaka jana, lilimuorodhesha miongoni mwa
matajiri 40 Afrika kwamba anamiliki utajiri wenye thamani
ya dola milioni 620 (karibu shilingi trilioni moja). Hata
hivyo, inadaiwa kuwa tabia ya usiri wa Bakhresa inafanya
mali zake zisijulikane sana, ila ni tajiri zaidi ya kiwango
hicho.
Ndiye mmiliki wa makampuni ya Bakhresa yanayotoa
bidhaa zenye chapa ya Azam ambazo zinauzwa nchi
mbalimbali Afrika. Ana viwanda vya nafaka na vinywaji,
vyombo vya usafiri wa majini, uuzaji wa chakula, bidhaa za
plastiki na kadhalika. Ndiye mmiliki wa Klabu ya Azam FC.
2. GULAM DEWJI
Huyu ni baba wa mfanyabiashara maarufu nchini,
Mohamed Dewji ‘Mo’. Jarida la Forbes mwaka jana lilimtaja
kuwa na utajiri wenye thamani ya dola milioni 560 (karibu
shilingi bilioni 900). Mafanikio yake kibiashara yalianza
mwaka 1970. Kiwanda chake cha 21st Century Textiles,
kinatajwa kuwa moja ya viwanda vikubwa vya nguo Afrika.
3. ROSTAM AZIZ
Inadaiwa anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni
420 (shilingi bilioni 672). Anamiliki karibu asilimia 40 ya
hisa Kampuni ya Vodacom Tanzania. Ni mmiliki wa
Kampuni ya Caspian inayohusika na uchimbaji wa madini
na ukandarasi nchini Tanzania, nchi kadhaa za Afrika na
Asia.
4. DK. REGINALD MENGI
Anatajwa kumiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni
280 (karibu shilingi bilioni 450). Ni mmiliki wa kundi la
makampuni ya IPP, yanayomiliki vyombo vya habari,
viwanda, migodi ya dhahabu, Tanzanite na kadhalika.
5. ALI MUFURUKI
Utajiri wake unatajwa kuwa na thamani ya dola milioni 110
(shilingi bilioni 176). Ni mmiliki wa kundi la makumpuni
ya Infortech Investment, inayomiliki maduka yanayouza
vitu vya rejareja Tanzania na Uganda. Vilevile ana vitega
uchumi vingine.
6. MUSTAFA SABODO
Ni mfayabiashara mkubwa sana nchini anayemwaga
mamilioni kwa misaada. Wakati wa kuanzishwa kwake,
aliipa Taasisi ya Mwalimu Nyerere shilingi milioni 800,
akasaidia shilingi milioni 100 katika mradi wa kustawisha
mimea jamii ya kunde. Vilevile alikipa Chadema shilingi
milioni 300. Inadaiwa kuwa utajiri wake unazidi shilingi
bilioni 100. Kampuni yake ya Khoja Shia Itnasheri Jamat
(KSIJ), ndiyo yeye tenda ya kujenga maeneo ya maegesho ya
magari Posta, Dar es Salaam, mradi wenye thamani ya
shilingi bilioni 5.6.
7. ABDUL-AZIZ ABOOD
Kiwango chake cha utajiri hakiwekwi sana wazi lakini
anatajwa kuwa miongoni mwa mabilionea 10 wanaotikisa
nchi kwa sasa. Anamiliki viwanda kadhaa mkoani
Morogoro, vyombo vya habari, Abood Radio na TV.
Anamiliki mabasi ambayo yanafanya safari zake kati ya
Morogoro, Mbeya na Dar es Salaam. Ni Mbunge wa
Morogoro Mjini (CCM).
8. MICHAEL SHIRIMA
Ni mmiliki mkuu wa Shirika la Ndege la Precision ambalo
linafaya safari zake ndani ya Tanzania pamoja na nchi
mbalimbali za Afrika. Ana asilimia tano ya hisa katika Beki
ya I&M (Tanzania), vilevile ni memba katika bodi ya
wakurugenzi wa benki hiyo yenye thamani ta shilingi
bilioni 200. Hisa zake Precision ni asilimia 42.91.
9. YUSUF MANJI
Kiwango halisi cha utajiri wake bado hakifahamiki lakini
anafahamika kama mmoja wa mabilionea wakubwa nchini
Tanzania. Ni mmiliki wa makampuni ya Quality Group na
majengo ya Quality Centre, Quality Plaza na kadhalika. Ni
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga na utajiri wake umeifaya
timu kutotetereka tangu alipoanza kuiongoza.
10. MOHAMMED DEWJI
Baba yake anashika nafasi ya pili katika orodha hii. Dewji
au Mo kama anavyoitwa na wengi, anatajwa kuwa bilionea
nambari moja katika orodha ya mabilionea vijana Afrika
(orodha hiyo tuliitoa wiki iliyopita). Ni mmiliki wa
makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited
(METL) ambayo inatengeneza faida ya shilingi bilioni 136
kwa mwaka

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana