Featured

    Featured Posts

NYUMBA YA MWENYEKITI MWENZA WA UKAWA JAMES MBATIA YATEKETEA KWA MOTO


Yadaiwa kuwa sababu ni hitilafu ya umeme

Nyumba ya makazi ya mwenyekiti wa chama cha NCCR-MAGEUZI,JAMES MBATIA,imeteketea kwa moto jana majira ya saa saba unusu mchana , kwa kile kilichoelezwa kuwa huenda ni hitilafu ya umeme unaosemekana kukatika asubuhi na kurejea mchana kwa kasi zaidi.

Akizungumza ,kaka wa James Mbatia FELIX KESSI,amesema hadi sasa wanachoweza kueleza ni uharibifu uliotokea kutokana na moto huo , kwani hawakuwepo wakati wa tukio , ingawa anawashukuru majirani walioweza kuokoa baadhi ya vitu vya ndani.

Amesema ni mapema mno kuzungumzia aina ya uharibifu kwani atakayeweza kujua zaidi ni mkewe na Mbatia ambae kwa wakati huo, haikuweza kuzungumza naye, kufuatia kupandwa na shinikizo la damu kutokana na tukio hilo .

Kwa upande wake mkuu wa oparesheni hiyo kutoka kikosi cha zima moto na uokoaji kwa wakati huo nyumbani hapo sajenti HAJI MADULIKA, amesema kikosi chake kiliwahi eneo la tukio ingawa kutokana na ukubwa wa moto, walishindwa kuokoa baadhi ya vitu, aidha ameoneshwa kushangazwa kwake na tabia ya watu kuwashutumu askari wa zimamoto kwa kuchelewa huku wanacnhi wakielewa hali halisi ya barabara.
CHANZO: CHANNEL TEN
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana