Featured

    Featured Posts

MFAHAMU MDADA MWANAHARAKATI ALIE AMUA KUJITANGAZA KUA AMEATHIRIKA NA UKIMWI NA KUBADILI MTAZAMO WA WENGI KUHUSU UGONJWA HUO.


Bi Phindile Sithole-Spong, mdada aliyejitangaza kua ameathrika na ukimwi.

Kama anavyo onekana kwenye picha hapo juu, Bi Phindile Sithole-Spong ni mwanaharakati kutoka Afrika Kusini anayeishi na virusi vya Ukimwi, amekuwa akiongoza juhudi za kukabiliana na unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi na hususan miongoni mwa vijana.
Mwanamke huyu aligundua akiwa na miaka kumi na tisa kwamba alizaliwa na ugonjwa wa Ukimwi, Phindile alijihusisha na usambazaji wa ujumbe kuhusu Ukimwi na Afya ya Uzazi, hasa maeneo ya kusini mwa Afrika, ambayo yameathirika pakubwa na Ukimwi.
Bi Sithole-Spong, alizindua kampeni ya Rebranding HIV mwaka 2013 kubadili mtazamo wa jamii kuhusu virusi vya Ukimwi, hasa miongoni mwa vijana akiwa katika chuo kikuu cha Cape Town.
Nchini Afrika Kusini takriban asilimia 11.2 ya raia wote wanaishi na virusi vya Ukimwi.
Kwa sasa, Bi Sithole-Spong ni mshauri wa mashirika makubwa ya kimataifa kama vile Muungano wa Afrika na UNAIDS.

Bi Phindile Sithole-Spong.

Baada ya kufahamu kuwa watu wa rika lake, familia na marafiki walikuwa wameathirika na janga la Ukimwi duniani pamoja na kuongezeka kwa maambukizi mapya nchini Afrika Kusini, licha ya kampeni mbalimbali, Phindile amekuwa akijihusisha na kampeni ya kuendeleza mtazamo chanya kuhusu Ukimwi na Afya ya Uzazi.
''Nina fahari sana moyoni kwa vijana ambao hawaaibiki kuishi na Ukimwi. Sote tunakumbwa na Ukimwi kila siku kama vijana, huwezi kutambua kama mtu ana Ukimwi au la, ni kama tu magonjwa mengine kwa sababu unaweza kujitibu,” anasema.
Kwa harakati zake za kuhamasisha mtazamo mwema kwa watu katika jamii zinazoathirika na janga la Ukimwi, amepongezwa sana.
“Ninafanya kitu ambacho ninakipenda sana. Huwa sihisi kwamba ni kazi. Sijilazimishi. Kwa mfano huwa siandiki hotuba zangu,” anasema.
"Huwa zinatoka katika sehemu halisi moyoni mwangu ambayo ina hamu ya kutaka kusaidia. Ya kutaka kupaza sauti yangu popote inapoweza.”

 
Bi Phindile Sithole-Spong.

Mwongozo mpya wa matibabu ya UKIMWI toka WHO,

Logo ya Shirika la Afya Duniani (WHO).

Shirika la Afya Duniani (WHO) limebadili msimamo wake wa awali ambapo walioathirika na virusi vinavyosababisha ukimwi (HIV) ilibidi wasubiri kuwa wagonjwa kabisa kabla ya kuanza kutumia tembe za kupunguza makali ya ukimwi.
WHO limeagiza kuwa kila mtu anayethibitishwa kuwa ameambukizwa na virusi vinavyosababisha ukimwi, HIV, anapaswa kuanza kupewa matibabu mara moja.
Mwongozo huu mpya unatokana na ushahidi unaoonyesha kuwa watu walio na HIV wanaoanza kutibiwa mara moja huishi kwa muda mrefu zaidi.
WHO linaamini kuwa mwongozo huu mpya unaweza kupunguza vifo zaidi ya milioni 21 kwa muda wa miongo miwili ijayo.


ARVS, dawa za kupunguza makali ya UKIMWI.

Ushahidi uliopatikana katika mataifa yanayostawi kama vile Marekani uanonyesha kuwa wagonjwa wengi wanaoanza kutibiwa tu mara wanapogunduliwa kuwa na virusi vya ukimwi huishi muda mrefu zaidi.
Shirika hilo pia linapendekeza kwamba makundi ya watu ambao wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa wanapaswa kupewa nafasi ya kwanza kutibiwa hata kabla ya uchunguzi kufanywa.
Muongozo mpya uliotolewa unamaanisha kuwa watu milioni 37 kote duniani ambao wanauguwa UKIMWI wanapaswa kupewa dawa za kupunguza makali ya ukimwi
Kwa sasa, watu milioni 15 tu ndio wanapata dawa hizo kote duniani.
Ushauri wa shirika hilo umeungwa mkono na mashirika ya kutoa misaada ya matibabu.
Hata hivyo shirika hilo limesema kuwa kutibu wagonjwa wengi wapya kutahitaji fedha za ziada.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana