"Ndugu zangu,
Naomba niwakumbushe jambo moja kubwa na la msingi ambalo labda mmelisahau. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na inaruhusu kila mtanzania kuwa na imani yake ya kisiasa, kwani ni haki yake ya msingi.
Kiukweli nasikitishwa sana na hii tabia ya watu kuamini kwamba vijana wanaokiunga mkono chama tawala wamenunuliwa, wanatukanwa kila siku na kudhalilishwa kana kwamba hawana haki kwenye nchi yao.
Mbaya zaidi sasa tunaelekea kwenye kupandikizwa ugomvi na viongozi wetu wa chama, najiuliza ili iweje?
Ndio demokrasia hiyo?
Jioni ya leo kuna clip ya kutengenezwa, imewekwa, eti mimi nagombana na Katibu Mwenezi wa CCM, hicho kitu hakijawahi kutokea, sisi hatuna tofauti, najiuliza sasa haya yote yanatoka wapi?
Kwa nini tusiongee sera tukabaki kwenye kuamua kumpigia tunayemtaka?
Kuna wakati kaka yetu ambaye ni Mwandishi wa muda mrefu Mdimuz aliwahi kuandika twitter kwamba kuna demokrasia ya mihemko, nikawa sijamuelewa leo ndio nimemuelewa, tuongee hoja za msingi, tujibu kwa hoja matusi tusiyape nafasi wala kuchafuana.
Kuna maisha baada ya uchaguzi, tusije kushindwa kuangaliana usoni na hii mihemko yetu na jazba tunazozipa nafasi mpaka tunapandikizana mauongo.
Mungu atubariki sana sisi watanzania na amani yetu iliyo katika hatari ya kuchafuliwa na wasiojielewa", Aunt Ezekiel ameandika kwenye ukursa wake wa Instagram

Toka jana clip yenye sauti inayodaiwa ni kuwa ya Aunt Ezekiel ikimtolea maneno machafu Nape imekuwa ikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii hususani Whatsapp
Post a Comment