:Jaji Mkuu wa Mashindano ya Bongo Star Search ‘BSS’, Ritha Poulsen ‘Madam Ritha’, akielezea mipango ya fainali ya mashindano hayo itakavyokuwa siku ya Ijumaa Oktoba 9 mwaka huu katika Ukumbi wa King Solomon Hall uliopo eneo la Namanga Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa washiriki wa shindano hilo, Nassib Fonabo, akiimba kwenye kikao hicho.
Angel Kato ambaye ni mshiriki wa shindano hilo, akiimba mbele ya waandishi wa habari.
Mshiriki wa shindano hilo, Frida Amani, ‘akichana’ mistari mbele ya waandishi wa habari.
Madam Ritha akiwatambulisha washiriki.
SHINDANO la kusaka vipaji vya muziki, Bongo Star Search (BSS) linalotarajiwa kufanyika Oktoba 9, limeongeza zawadi ya mshindi wa shindano hilo ambapo sasa atajinyakulia shilingi milioni 60, ambapo shilingi milioni kumi zitapelekwa studio kwa ajili ya kusaidia shughuli za kurekodi.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Jaji Mkuu wa shindano hilo Ritha Paulsen ‘Madam Ritha’, alisema kuwa shindano hilo lina msisimuko wa kipekee kwa kuwa washiriki wote ni wazuri kiasi majaji wanapata wakati mgumu kumchagua mshindi.
“Mshindi wa shindano hili ataondoka na sh. milioni 60, katika kinyang’anyiro cha safari hii chenye msisimko mkubwa hadi hata sisi wenyewe tunapata wakati mgumu kama majaji,” alisema Ritha
Fainali za shindano hilo zinatarajiwa kufanyika Ijumaa Oktoba 9 Mwaka huu katika Ukumbi wa King Solomon uliopo eneo la Namanga Kinondoni jijini Dar es Salaam. Siku hiyo pia kutakuwa na burudani za nguvu kutoka kwa msanii Run Town wa Nigeria ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Gallardo.
“Ukiachia mbali msanii huyo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa Christian Bella, Yamoto Bendi, Nevy Kenzo ambao watakamua sambamba na wasanii mahiri ambao ni zao la BSS kama Peter Msechu na Kala Jeremiah. Viingilio siku hiyo vitakuwa 25,000/=, ambapo nafasi za VIP zitakuwa 50,000/= na viti maalum vitalipiwa 100,000/=. Nawaomba mashabiki waje kwa wingi maana fainali ya mwaka huu ni ya kipekee kabisa,” alisema Madam Ritha.
Post a Comment