Mkali wa maigizo kutoka kiwanda cha filamu bongo Rose Ndauka, amefunguka kuwa tabia ya baadhi ya watu kumshutumu msanii mwenzie wa filamu Elizabeth Michael “Lulu” si nzuri na inaweza kusababisha matatizo katika mwenendo wa maisha yake.
Kauli ya Rose inakuja siku moja baada ya kifo cha mfanya biashara na mdau wa tasnia ya burudani bongo marehemu Lusekelo Samson Mwandenga, kwa kile kinachodaiwa marehemu alikuwa na uhusiano na mwigizaji huyo.
“Lulu ni binti mdogo ambaye amepitia matatizo mengi sana kwenye maisha, jamni tatizo linaloweza kumpata mwenzako hata wewe linaweza kukupata tuwe wenye Imani muda mwingine wa kumuombea mwenzetu anapopata matatizo” ameandika Rose Instagram.
Shutuma hizo zinazotoka kwa baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii zinausishwa na tukio la kifo cha muigizaji nguli Steven Charles Kanumba, april 7 2012 ambapo alifariki kwa kusukumwa na aliyekua mpenzi wake Elizabeth Michael “LULU”.
Mungu ailaze roho ya marehemu Lusekelo “secki” mahala pema peponi Amin.
Post a Comment