HABARI zilizotufikia muda huu zinasema Waziri wa Uchukuzi, Samwel Siita, amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini, Madeni Kipande, kutokana na matumizi mabaya ya ofisi yaliyoisababishia serikali hasara ya mabilioni ya shilingi.
Kusimamishwa kwa Kipande kunatokana na vyombo vya habari kufichua ufisadi uliokuwa unafanywa na mkurugenzi huyo ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha wafanyakazi kinyume na taratibu na sheria.
Kashfa nyingine inayomsakama Kipande ni kuruhusu watu waliosimamishwa kazi bandarini kwa zaidi ya miaka miwili kuendelea kupokea mishahara na marupurupu kama kawaida.
Post a Comment