Featured

    Featured Posts

UMEIPATA HII YA KIJANA KUZAMIA KWENYE TAIRI ZA NDEGE? IKO HAPA

Moja ya story zilizokuwa kubwa sana miaka ya nyuma ilikuwa ni watu mbalimbali hasa vijana kufanya uzamiaji kwa njia ya  meli, inafaamika kama stowaway kwa lengo la kwenda nchi za Ulaya, Marekani, Afrika Kusini na nyinginezo, vijana walikuwa wakifanya hivi kwa lengo la kutafuta maisha mazuri.

Hii imesikika sana nchi za Kaskazini mwa Afrika, Tunisia ikiwa ni mojawapo ambapo mpaka hivi sasa kumekuwa na wazamiaji wakielekea Ulaya kutafuta maisha mazuri, lakini kutoka uwanja wa ndege wa Murtala Muhammed, Lagos Nigeria, kijana mdogo amekutwa akiwa amejificha ndani ya sehemu zinakoingia tairi za ndege moja ya kukodi iliyokuwa uwanjani hapo.

Ndege hiyo inamilikiwa na shirika la ndege la Tag Aviation ilikuwa imeegeshwa huku marubani wakifanya ukaguzi kabla ya kuwasha engine ndipo walipomkuta kijana huyo akiwa na simu mbili za mkononi ambazo hazikuwa na line.

Kijana huyo alisema kuwa aliingia kwenye ndege hiyo kwa kupitia jengo la idara ya Nigeria Air Force karibu na mlango wa VIP wanakoingilia viongozi kama Marais.

Amesema kuwa alifanikiwa kuingia kwenye sehemu hiyo ya tairi za ndege kwa kusaidiwa na kaka yake.

Tukio kama hili liliwahi kutokea mwaka 2013 Nigeria, Daniel Ihekima ambaye alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Lagos baada ya kukutwa sehemu ya tairi kwenye ndege ya Arik Plane lakini yeye alifanikiwa kusafiri kutoka Benin hadi Lagos, ndege ilipotua alijua yuko Marekani.

Daniel Ihekima

Hapa kuna video ya John Legend aliyoifanya Zanzibar mwaka 2007, ilikuwa dedication kwa watoto wawili, Yaguine Koita na Fode Tounkara ambao walifariki baada ya kuzamia kwenye tairi ya ndege kutoka Guinea kwenda Ubelgiji mwaka 1999.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana