Hakuna anebisha kuwa mrembo na mwigizaji wa filamu Diana Elizabeth Michael ‘Lulu’ni moja kati ya mastaa wanaokwenda na fasheni na huwa hakosei kwenye hili, yaani huyu yupo “on point”.
Lakini linapokuja swala la maadili na utamaduni wetu hapa watu ndio huwa hutofautiana juu ya mavazi wanaoyovaa dada zetu siku hizi.
Picha za mwanadada Lulu akiwa amevalia kivazi ambacho kwa kiasi kikubwa kimeacha miguu yake wazi zilisambaa kwa kasi sana mtandao hapo jana, hii ni kutokana na wengi kuzi LIKE na ku-SHARE.
Kama kawaida yetu wa bantu, japokuwa wengi walitupia COMMENTS za kumsifia wengine pia waliponda uvaaji wa kanguo hako, na wengine kuanza kumtio kasoro, mbali na yeye mwenye Lulu kuandika mamaneno haya kwenye moja kati ya picha hizo.
“Sema nini.....tumiguu twangu tumenyooka hatuna kona...chaiiiii.. Na tumatege flani amaizing …Usinipanikie Mimi Lakini”by Lulu.
Kwa mtazamo wangu kwanza kabisa ni ukweli Lulu DIVA waukweli hapa mjini, sasa hilo swala la mavazi gani ndio ya maadili nawaachia nyie, mnalionaje hapa
Jionee picha hizo akiwa na kavazi hako hapo juu
Post a Comment