Mwili wa Marehemu Huma Simon ukiwa eneo la tukio
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Huma Simon (27) mkazi wa kitongoji cha Solwa Kata ya Solwa Wilayani Shinyanga Vijijini ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.
Kwa mujibu wa Majirani Mwili wa marehemu Huma umekutwa asubuhi katika eneo la Shule ya msingi Solwa ukiwa umekatwa mapanga sehemu mbalimbali na kutelekezwa.
Taarifa zimesema Huma ambaye anaishi na Mama yake Mzazi, alitoka usiku katika chumba alichokua amelala na kumuacha Mtoto wake wa kike anayekadiriwa kuwa na miaka miwili, na kukutwa asubuhi akiwa ameuawa.
Mama wa marehemu
Post a Comment