Featured

    Featured Posts

BINTI MCHAWI ANASA KWENYE NYUMBA AKIWA ANA WANGA HUKO SHINYANGA MJINI

 


Siku chache tu baada ya bibi aliyedhaniwa kuwa mchawi mwenye umri wa miaka 80 kukutwa nje ya nyumba ya mtu akiwa uchi huku Ndembeza mjini Shinyanga leo binti binti anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 23- 25 anayedaiwa kuwa ni mchawi amekutwa kwenye nyumba ya mtu katika mtaa wa Bushushu kata ya Lubaga katika manispaa ya Shinyanga akiwa amevaa kishirikina huku mwili wake ukiwa umepakwa dawa nyeusi akidai alikuwa anaongoza wenzake zaidi ya 10 Geita,Mwanza na Shinyanga kuwanga katika nyumba hiyo . 

Mguu wa binti huyo aliyedai kutoka Ushirombo.
Tukio hili limetokea leo asubuhi katika mtaa wa Bushushu nyumbani kwa Robinson Massawe ambapo binti huyo alikutwa amelala mbele ya mlango wa nyumba hiyo akiwa hajitambui na baada ya kusemeshwa ndipo akasimulia yaliyomkuta kwamba alifika mahali hapo na wenzake zaidi ya 10 kutoka kanda ya ziwa kufanya sherehe baada ya kufanikisha uchawi wao wa kuharibu ndoa ya Massawe. 

Askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakimhoji binti huyo
ambapo baada ya kumhoji binti huyo alisema alifika kwenye familia hiyo,akiwa kiongozi wa kundi la wachawi zaidi ya 10 kutoka Ushirombo,Misungwi na Shinyanga saa 9 usiku kwa ajili ya kufanya sherehe baada ya kufanikiwa kusambaratisha kichawi ndoa ya Massawe na Mary Joseph.

Anasema leo ni mara ya tatu wanakuja kufanya uchawi wao,lengo lao ni kutaka ndugu yao aolewe na Massawe,walikuja siku ya kwanza wakakuta mke wa Massawe akisali,wakashindwa,wakarudi mara ya pili kwa ajili ya kusambaratisha ndoa,wakafanikiwa leo walikuja kufanya sherehe kwa kazi hiyo lakini wenzake wamemkimbia.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana