Featured

    Featured Posts

WASTARA KUMUANIKA MRITHI WA SAJUKI

Staa wa filamu Bongo, Wastara Juma. 

Stori: Imelda Mtema
STAA wa filamu Bongo, Wastara Juma, ametamka hadharani kuwa hana uhusiano wa kimapenzi na msanii yeyote ndani ya Kundi la Bongo Movie. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Wastara alisema kuna maneno mengi yanasemwa kuwa ana uhusiano na mtu ndani ya kundi hilo kitu ambacho si sahihi, atamuanika mrithi wa marehemu Sajuki siku si nyingi. 

“Unajua muda utafika tu lakini kwa hivi sasa sina bwana wala sihitaji mtu yeyote ndani ya Kundi la Bongo Movie na mtu ambaye ataishi na mimi muda ukifika nitawatambulisha na kila mmoja atamjua na siyo mtu kunitabiria au kubuni nitamuweka wazi muda si mrefu,” alisema Wastara.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana