MVUA ya muda mfupi iliyonyesha jijini Dar es Salaam na maeneo ya jirani asubuhi ya leo iliyaacha maeneo mengi yakiwa yamejaa maji na kusababisha shida kubwa kwa wakazi wa jiji hili. Baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na kadhia hiyo ni Bamaga-Mwenge ambako mitaro yenye kusafirisha maji ilijaa na maji kufurika hadi katika barabara na kufanya magari na waenda kwa miguu kupata shida.
Post a Comment