Featured

    Featured Posts

MARA BAADA YA MUHONGO KUJIUZULU NA JK KUTEUA WAPYA, ZITTO ATOA YA MAYONI!



Kufuatia hatua  ya Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Sospeter Muhongo kujiuzulu katika  nafasi  hiyo ya  uwaziri,  mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mh Zitto Kabwe amepongeza uamuzi huo wa Prof Muhongo ambapo amesema kuwa hatua hiyo ni heshima kubwa kwa bunge.
 
"Napenda kuchukua nafasi hii kutambua busara aliyochukua ambayo naamini itasaidia harakati za kujenga demokrasia yenye uwajibikaji. 
 
"Naamini uamuzi wa Ndugu Muhongo umewezesha kulinda heshima ya Bunge na maazimio yake. Kwa muda mfupi alioongoza Wizara hiyo, Ndugu Muhongo ameweza kuongoza mabadiliko kadhaa muhimu ya kiutendaji katika wizara hiyo na taasisi zake. 
 
"Hata hivyo, nafasi ya Wizara aliyokuwa anaongoza katika suala la Tegeta Escrowimemtia doa kubwa ambalo ilikuwa lazima awajibike. 
 
"Naamini Rais Kikwete atamteua mtu mchapakazi na makini zaidi atakayeweza kuendeleza yale mazuri ya Ndugu Muhongo na kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza." Amesema Zitto kupitia ukurasa wake wa Facebook.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana