Featured

    Featured Posts

Kumbe mtoto wa Cristiano Ronaldo ni shabiki wa Lionel Messi? Cheki kwenye video hapa walipokutana

Katika miaka takribani 10 iliyopita ulimwengu wa soka umetawaliwa na upinzani wa jadi katika ya wanasoka wawili bora kabisa katika kizazi hiki, Mreno CristianoRonaldo na Lionel Messi. 

Lakini pamoja na upinzani walionao uwanjani, wanasoka hao wawili wameonyesha kuwa na uhusiano mzuri wanapokuwa nje ya uwanja, kwa pamoja wawili hao walionyesha hilo wakati walipokuwa Uswisi mwanzoni mwa wiki hii kwenye sherehe za utoaji tuzo ya Ballon d’Or. 

Katika kuonyesha hawana uadui, imetolewa video inayomuonyesha Cristiano Ronaldo  akimwambia Lionel Messi kwamba mwanae ambaye ni Cristiano JR ni shabiki wake mkubwa. 

Alikaririwa akimwambia: “Mwanangu anakupenda sana, muda wote anaangalia video zako kwenye mtandao wa intaneti“– Cristiano Ronaldo. Angalia video yenyewe hapo chini
 

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana