Featured

    Featured Posts

Manchester United Agree £31m Deal For Benfica Defender | Read Full Details

Victor Lindelof
Manchester United have agreed a deal to sign Sweden defender Victor Lindelof from Benfica for £31m (35m euros).
United say the deal is now subject to international clearance, the agreement of personal terms and a medical, which will take place next week.
Lindelof, who has been capped 12 times by his country, is due to play in a friendly in Norway on Tuesday.
The 22-year-old centre-back, who has been with Benfica since 2012, will be United’s first signing of the summer.
Lindelof made 47 appearances for the Portuguese side last season, helping them win a domestic league and cup double.

SAMATTA ATOA YA MOYONI KUHUSU KICHAPO CHA TANZANIA KUPIGWA BAO 7


Nyota wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta ameandika kwenye account yake ya facebook kuonesha masikitiko yake baada ya Stars kupokea kichapo cha magoli 7-0 mbele ya Algeria kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi uliochezwa jana usiku kwenye mji wa Blida, Algeria.
Samatta amesema inaumiza sana pale anapoingia wanjani kutafuta ushindi lakini mambo yanakuwa tofauti na vile anavyotarajia huku kukiwa na idadi kubwa ya watu wanatumaini mazuri huku wakitoa sapoti yao kwa kila hali.
“Matokeo yalikuwa mabaya sana, wote yametuumiza, na inauma sana unapokuwa uwanjani ukijitahidi kufanya kila liwezekanalo lakini mambo hayaendi sawa na huku ukijua kuna mamilioni ya watu wanaotumaini mazuri yafanyike na wanatoa sapoti yao”, Samatta ameandika kwenye account yake ya facebook.
“Kushindwa michuano ni sawa na unaposhindwa vita, unaweza ukaamua kukata tamaa kabisa na kufia uwanja wa mapanbano au unaweza kukubali kushindwa kabla matumaini hayajafa uka-retreat ili ujipange upya”.
“Mimi naiamini option ya pili ndio option ambayo inafanya ndoto ziendelee kuishi na maisha yaendelee. Ninameza maumivu na kuendelea na safari japo hayatokata kiu ila muhimu ni kupita kwenye kipindi kigumu kama hiki. Kushindwa sio silaha ya kutokomeza imani, ila ni teke linalompa maumivu chura na kumfanya atafute njia nyingine ya kupita mpaka afike safari yake”.

LIGI KUU ENGLAND : MAN UTD YAICHAPA TOTTENHAM



Manchester United new boy Memphis Depay (centre) congratulates Wayne Rooney as the home side take a 1-0 lead
Jan Vertonghen (left) looks to the turf as Rooney is joined by Depay and Juan Mata in celebration of United's opener

United's new No 7 Depay, who started brightly on his Premier League debut, revels in the opening goal celebrations
Tottenham came close to taking an early 1-0 lead through Christian Eriksen, but the Danish star lofted his effort just over the crossbar
Spurs winger Eriksen reacts after seeing his effort drift agonisingly over Sergio Romero's bar during the first 45 minutes 
Matteo Darmian (left) gets to grips with Spurs star Harry Kane as Mauricio Pochettino's side impose themselves at Old Trafford 
Spurs defender Kyle Walker inadvertently taps the ball into his own net while attempting to tackle Rooney 

+30

Rooney found himself in space inside the Spurs penalty area before Walker robbed him of the ball and pushed the ball past Michel Vorm


HUYU NDIYE MRITHI WA VAN PERSIE

Klabu ya Manchester United imemuuza straika wake namba moja Robin Van Persie kwenda klabu ya Fernabache. 
Tayari wachambuzi wa soka wameeanza kuyataja majina ya mastraika ambao wanaweza kusajiliwa na Man United kama mbadala wa Van Persie

HARRY KANE
Wachezaji wachache wamekuwa na mafanikio msimu kama Muingereza huyu anayecheza kwenye timu ya Uingereza yenye chini ya miaka 21. Ni Sergio Aguero pekee ndiye aliyefunga mabao zaidi Ligi Kuu kuliko Kane msimu uliopita. Kane amefunga mabao 21. Luis Van Gaal yupo tayari kulipa £ 50,000,000 kwa ajili ya Kane ingawaje Tottenham wamesema kuwa hawapo tayari kumuuza.

MULLER
Muller ameonekana hakuridhika kabisa na jukumu alilopewa kulifanya pale Munich msimu uliopita ingawaje bado anabaki kuwa hazina kubwa kwa timu hiyo. Ripoti zinasema kuwa Van Gaal yupo tayari kulipa jumla £ 120m kwa ajili ya Muller.
BENZEMA
Mpango Rafa Benitez wa kutaka kumchezesha Cristiano Ronaldo mbele kama namba 9 kunaweza kukamfanya Mfaransa kutaka kuondoka klabuni hapo. Ripoti zinadai kuwa LVG yupo tayari kulipia huduma ya Mfaransa huyo.

CAVANNI
Bado Cavanni hajaweza kabisa kumzidi Zlatan Ibrahimovic kama straika chaguo namba moja klabuni PSG. Kuna hisia kuwa Cavanni hafurahii maisha yake kule Ufaransa hivyo yupo tayari kuondoka muda wowote.

LEWANDOWSKI
Man United tayari wameshaini mchezaji mmoja kutoka Bayern (Bastian Schweinsteiger) na ripoti zinasema kuwa inawezekana Man United wakahitaji saini ya mchezaji huyu ingawaje Bayern wameshasema kuwa hawawezi tena kumruhusu mchezaji wao yeyote kujiunga tena na klabu hiyo msimu huu.
BERAINO
Kijana huyu wa West Brom tayari ameshavutia klabu nyingi kubwa barani Ulaya kama Liverpool na Man United. Kama wachezaji wakubwa aliopanga kuwasajili atashindwa, basi LVG anaweza kumsajili kinda huyu.
BENTEKE
Mbelgiji huyu yupo zaidi kwenye rada za Liverpool ingawaje ripoti zinasema kuwa hata Man United wanamvizia kwa karibu sana.

HIGUANI
Murgentina huyu amekuwa akihusishwa na timu za Uingereza kwa muda mrefu sasa. Na baada ya Napoli kushindwa kufuzu UEFA na kumpoteza kocha wao Rafa Benitez basi kuna uwezekano mkubwa wa yeye kujiunga na timu za Uingereza na tayari Man United wameshaonesha nia ya kumtaka.
LACAZETTE
ni Messi na Ronaldo ndio wamemzidi magoli mchezaji huyu kwa msimu uliopita. Hali imevifanya vilabu vikubwa kuanza kunyemelea saini ya mchezaji huyu anyekipiga katika klabu ya Lyon ya Ufaransa.

HAYA NDIYO MAISHA MAPYA YA NYOTA MRISHO NGASSA, HUKO SOUTH AFRIKA

Mshambuliaji mpya wa Free State Stars ya Afrika Kusini, Mrisho Khalfan Ngassa akiwa mbele ya gari la kutumia alilopewa na klabu yake hiyo baada ya kuwasili mjini Bethlehem leo yalipo makao makuu ya klabu hiyo ya Ligi Kuu ya nchini humo
Mke wa Ngassa, Radhia Mngazija akiwa jikoni kwenye nyumba yao baada ya kuingia leo

Radhia 'Nish' akiwa mlango wa nyuma wa nyumba yao mjini Bethlehem
Mrisho akiwa kwenye sebule ya nyumba yake mjini Bethlehem


Mrisho Ngassa akiwa mlango wa nyuma wa nyumba yao
Nyumba ipo barabarani kabisa
Nish akiwa kwenye geti la mbele la nyumba yao mjini Bethlehem

MKWASA ATANGAZAKIKOSI CHA TAIFA STARS, MAAMUZI MAGUMU YATUMIKA

Kocha mpya wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa aliyechukua nafasi ya Mart Nooij ametangaza kikosi chake kipya kwa ajili ya kuivaa Uganda huku akimtema kipa Deogratius Munish ‘Dida’ na nafasi yake amemchagua Ally Mustapha ‘Barthez’.
Wengine ambao Mkwasa amewatema ni Erasto Nyoni, Amri Kiemba na Kelvin Friday kutoka Azam FC pia Oscar Joshua kutoka Yanga, Pia Ibrahim Ajibu kutoka Simba.

Waliorejea ni Kelvin Yondani pia Deus Kaseke huku akimchukua Michael Idan wa Ruvu Shooting.
Pia Samuel Kamuntu wa JKT, Juma Abdul wa Yanga na Mudathir Yahya kutoka Azam wamejumuishwa kwamba wanaweza kuitwa wakati wowote.

KIKOSI KAMILI:
Mwadini Ally-Azam
Ally Mustapha-Yanga
Mudathir Khamis-KMKM
Shomari Kapombe-Azam
Michael Haidan-Ruvu Shooting
Mohammed Hussein-Simba
Mwinyi Hajj-KMKM
Nadir Haroub-Yanga
Kelvin Yondani-Yanga
Aggrey Morris-Azam
Hassan Isihaka-Simba
Jonas Mkude-Simba
Abdi Banda-Simba
Simon Msuva-Yanga
Said Ndemla-Simba
Ramadhan Singano-Simba
Salum Telela-Yanga
Frank Domayo-Azam
Atupele Green-Kagera Sugar
Rashid Mandawa-Mwadui
Ame Ally-Azam
Deus Kaseke-Yanga

TFF YAMFUKUZA KAZI KOCHA MKUU MAART NOOIJ KUINOA TAIFA STARS PAMOJA NA BENCHI ZIMA LA UFUNDI, BAADA YA UGANDA KUIFUNGA BAO 3-0 ZANZIBAR.



Kocha Mkuu wa Taifa Stars Maart Nooij akisindikizwa na ulinzi mkali usiku huu baada ya kumalizika kwa mchezo wa Tanzania na Uganda wa kuwania kufuzu fainali za CHAN katika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar ambapo Taifa Stars ilichapwa 3-0.
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha pamoja na mambo mengine kilipitia mwenendo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmini ya mwenendo wa timu.  
Kamati ya Utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo:
1. Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia Juni 21, 2015.

2. Benchi lote la ufundi la Taifa Stars limevunjwa kuanzia Juni 21, 2015.

3. Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Juni 20, 2015.

MRISHO NGASSA ASAJILIWA NA KLABU HII KUBWA NCHINI AFRIKA KUSINI



KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania
Mrisho Khalfan Ngassa amesaini Mkataba wa
miaka minne kujiunga na klabu ya Free State
Stars ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini leo.
Ngassa, mume wa Radhia na baba wa Farida (8)
na Faria (6) aliwasili jana jioni mjini hapa na leo
asubuhi baada ya kukamilisha mazungumzo,
akasaini Mkataba huo mnono.
“Nimefurahi kusaini timu hii, ambayo kaka yangu
Nteze John amewahi kuchezea pamoja na
wachezaji wengine wakubwa kama Tshabalala n
Mweene,”alisema Ngassa.
“Sasa najiandaa kwa maisha mapya baada ya
kucheza Tanzania kwa muda mrefu, hii ni
changamoto mpya kwangu, mpira wa Afrika
Kusini upo juu sana ukilinganisha na pale kwetu
(Tanzania). Nataka kutumia fursa hii kuitangaza
soka ya Tanzania, ili klabu zisijifikirie tena kusaji
wachezaji wa Tanzania,”amesema Ngassa.
Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa timu hiyo
maarufu kama Ea Lla Koto, Mmalawi Kinnah Phir
amesema kwamba amekuwa akimpenda Ngassa
kwa muda mrefu na kukutana naye FS ni kutimia
kwa ndoto zake za kufanya kazi na kijana huyo
siku moja.
Katika Mkataba huo ambao Ngassa, mtoto wa
kiungo wa zamani wa Simba SC, Khalfan Ngassa
atakuwa analipwa karibu mara tatu ya mshahar
aliokuwa anapata Yanga SC, atapatiwa nyumba
ya kuishi na familia yake, gari na huduma
nyingine muhimu, ikiwemo bima.
Ngassa anakuwa Mtanzania wa pili kuichezea
Free State, baada ya Nteze John Lungu ‘mwana
Mwanza’ pia aliyeichezea timu hiyo enzi hizo
inaitwa Qwa Qwa Stars mwaka 1997 hadi 1999.
Ngassa anatua Free States akitokea Yanga SC,
ambayo ameichezea jumla ya mechi 186 katika
awamu mbili, na kuifungia jumla ya mabao 86.
Ngassa aliyetimiza miaka 26, Aprili 12 mwaka
huu, alijiunga na Yanga SC kwa mara ya kwanza
mwaka 2006, akitokea Kagera Sugar iliyomuibua
mwaka 2005 kutoka timu ya vijana ya Toto
Africans ya Mwanza.
Mwaka 2010 alihamia Azam FC kwa dau la reko
wakati huo, dola za Kimarekani 40,000 (Sh.
Milioni 80).
Kabla ya hapo, akiwa Yanga SC, Aprili mwaka
2009, Ngassa alikwenda kufanya majaribio klabu
ya Ligi Kuu England, West Ham United wakati hu
chini ya kocha Mtaliano Gianfranco Zola.
Hata hivyo, pamoja na mshambuliaji wa zamani
wa Chelsea, Zola kuvutiwa na uwezo wa mcheza
huyo kisoka, akasema Ngassa anahitaji kurejea
Afrika kuongeza lishe.
Julai mwaka 2011, Ngassa alikwenda kufanya
majaribio Seattle Sounders FC ya Ligi Kuu ya
Marekani na akatumiwa katika mchezo wa
kujiandaa na msimu dhidi ya Manchester United
ya England.
Hata hivyo, Azam FC haikuwa tayari kumuuza
mchezaji huyo. Ngassa alicheza Azam FC hadi
mwaka 2012 alipohamia Simba SC kwa mkopo n
mwaka 2013 akarejea timu yake kipenzi, Yanga
SC ambayo, ameiaga baada ya msimu akiiachia
ubingwa wa Ligi Kuu.
Mfungaji huyo bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika
msimu uliopita, pia amewahi kuwa Mchezaji Bor
wa Tanzania mara mbili mwaka 2010.
Mwaka 2005 akiwa Kagera Sugar alishinda
Kombe la Tusker wakiifunga Simba SC katika
fainali na alipohamia Yanga SC alishinda mataji
ya Ligi Kuu katika misimu ya 2008, 2009 na
2015.
Ameshinda pia mataji ya Tusker mwaka 2007 na
2009 akiwa na Yanga SC, wakati akiwa na Azam
FC aliiwezesha timu hiyo kushika nafasi ya pili
katika Ligi Kuu na Klabu Bingwa Afrika Mashariki
na Kati, Kombe la Kagame mwaka 2012.
Amekuwa Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodaco
Tanzania Bara msimu wa 2010–2011 akiwa na
Azam FC na mfungaji bora wa Kombe la
Challenge mwaka 2009.
Huyo ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu mwezi
Apirli mwaka huu, ambaye ana nafasi kubwa ya
kuwa pia Mchezaji Bora wa jumla wa Ligin Kuu
msimu huu.
Amekuwa mchezaji muhimu wa timu ya taifa ya
Tanzania, Taifa Stars tangu mwaka 2007 na had
sasa amiechezea timu hiyo mechi 82 na kuifungi
mabao 22.

ANGALIA PICHA ZA FLOYD MAYWEATHE AKIJIFUA KWA NGUVU KUJINDAA NA PAMBANO LAKE

 

Bondia Floyd Mayweather amesema atapigana mara moja zaidi baada ya kupambana na Manny Pacquiao mwezi ujao, kwa sababu amesema hajisikii kuufurahia tena mchezo wa ndondi.
Mpambano wa Mayweather dhidi ya Pacquiao wa Mei 2 ni wa tano kati ya mapambano sita kwenye mkataba alioingia na shirika la utangazaji la Showtime
Mayweather, 38, amesema ile "furaha" haipo tena kwenye ndondi, na sasa anatazama fani hiyo kama "kazi" tu.
Amesema: "Sifurahii sana kama ilivyokuwa zamani. Pigano langu la mwisho ni Septemba."









SHUHUDIA JINSI BONDI MATUMLA WA TANZANIA ALIVYOMDUNDA BONDIA MCHINA


Mwamuzi wa Mpambano wa Masumbwi uliowakutanisha mabondia Mohamed Matumla (Tanzania) na Wang Xin Hua (China) katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam usiku huu,akiwa amemnyanyua mkono Bondia Mohamed Matumla baada ya kumchapa kwa Point bondia mwenzake kutoka nchini China katika mpambano wa raundi 10 wa kuwania nafasi ya kucheza katika pambano la utangulizi kwenye mpambano mkali na unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa masumbwi Duniani kati ya mabondia Floyd Mayweather, Jr. na Manny Pacquiao unakaochezwa mapeka mwezi Mei mwaka huu, huko nchini Marekani.
Wanahabari wakichukua taswira mbali mbali za mpambano huo.
Bondia Mohamed Matumla akiangalia namna ya kumrushia konde mpinzani wake Wang Xin Hua (China) wakati wa mpambano wao wa raundi 10 wa kuwania nafasi ya kucheza katika pambano la utangulizi kwenye mpambano mkali na unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa masumbwi Duniani kati ya mabondia Floyd Mayweather, Jr. na Manny Pacquiao unakaochezwa mapeka mwezi Mei mwaka huu, huko nchini Marekani.Katika Mpambano huu, Bondia Mohamed Matumla alishinda kwa point.
Matumla akimchezesha Wang Xin Hua.
Wang Xin Hua akirusha konde kwa Mohamed Matumla ambaye leo alikuwa makini sana kuhakikisha hampi point hata moja mpinzani wake.
Matumla anatakata hapa,anampa ambakati moja maridadi kabisa.

IVORY COAST YAPANDA KWA VIWANGO KATIKA ORODHA YA FIFA

IvoryCoast imepanda katika orodha ya shirikisho la soka duniani FIFA baada ya kushinda kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu.
Equitorial Guinea waandalizi wa kombe hilo pia walipanda na kuorodheshwa miongoni mwa mataifa 50 bora duniani.
Kikosi hicho kilipanda nafasi 69 na sasa kiko sawa na Congo katika nafasi ya 49 baada ya kufika nusu fainali ya mchuano huo ijapokuwa kwa utata.
Kikosi cha timu ya Algeria bado kinaongoza barani afrika kulingana na orodha mpya ya FIFA
Kikosi cha Ivory Coast kilipanda nafasi 8 juu hadi nafasi ya 20 ijapokuwa Algeria bado inasalia kuwa timu bora barani Afrika ikiwa katika nafasi ya 18..
Ndovu hao wameorodheshwa wa pili barani Afrika nyuma ya Desert Foxes,timu walioishinda katika robo fainali.
Timu ya Ghana ambayo ilicheza katika fainali ya kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya walioibuka washindi Ivory Coast imepanda nafasi 12 hadi nambari 25.
Ujerumani yaendelea kuongoza katika orodha mpya ya fifa baada ya kushinda kombe la dunia
Mataifa yalioshuka vibaya katika orodha hiyo barani Afrika ni Libya ilioshuka nafasi 35 hadi nambari 113 duniani.
Katika nafasi za kwanza ,Ujerumani bado inashikilia nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Argentina,Colombia,Belgium na Uholanzi katika nafasi ya 5.
Hakuna timu mpya zilizoingia katika orodha ya mataifa kumi 10 duniani.
Mataifa kumi bora barani Afrika: 1. Algeria 2. Ivory Coast 3. Ghana 4. Tunisia 5. Cape Verde 6. Senegal 7. Nigeria 8. Guinea 9. Cameroon 10. Congo DR
Mataifa kumi bora duniani 1. Germany 2. Argentina 3. Colombia 4. Belgium 5. Netherlands 6. Brazil 7. Portugal 8. France 9. Uruguay 10. Spain

MAPOKEZI YA TIMU YA IVORY COAST BAADA YA KUCHUKUA AFCON 2015 YAFANA

Huu ni umati mkubwa wa wananchi wa  Ivory Coast Jijini Abidjan Baada Ya Kutwaa Ubingwa-AFCON 2015. Nina uhakika ikitokea Tanzania tukachukua ubingwa huu itakua ni zaidi ya hapa



Hii ni baada ya kutwaa ubingwa huu waliokua wakiutafuta kwa muda mrefu. Hii ni mara ya pili kwa Ivory Coast kutwaa taji hili.

 



Kwa upande wao Ghana imekua ni kilio. Imekua ni vigumu sana kwa Adre Ayew kuamini kilichotokea na kujikuta akimwaga machozi muda mwingi baada ya kukosa taji.

Ayew was inconsolable after AFCON 2015 defeat

Kwa mara ya mwisho Ghana kuchukua ubingwa wa  AFCON ni 1982. Mwaka 1992 Ghana walikutana fainali na Ivory Coast pia na walishindwa kuchukua ubingwa. Mwaka huu 2015 walidhamiria kulipa kisasi kwa Ivory Coast lakini imeshindikana. Abedi Ayew Pele, baba yake dede,alikua ni miongoni mwa waliounda kikosi cha Ghana mwaka 1992 kilichoshindwa kunyakua ubingwa mbele ya Ivory Coast.

View image on Twitter

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana