HILI nalo janga! Mwanaume mmoja anayesemekana ni mfanyabiashara ambaye pia anatajwa kugombea udiwani wa kata moja iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, aliyetajwa kwa jina moja la mzee Beno amenaswa akiwa chumba cha gesti na denti wa chuo kimoja kilichopo Kibamba jijini Dar,
Tukio hilo la aina yake lilijiri Oktoba 20, mwaka huu ndani ya gesti moja (jina tunalo) iliyopo Kimara-Suka jijini Dar es Salaam ambako mama mzazi wa wa binti huyo ndiye aliyemnasa mheshimiwa mtarajiwa huyo na binti yake.
WASIWASI KWANZA
Awali, mama huyo alisema alianza kuwa na wasiwasi na mwenendo wa binti yake huyo kutokana na kuanza kale katabia ka’ kuchelewa mara kwa mara kurudi nyumbani akitoka chuoni, akajiongeza!
“Sisi tulishajua binti yetu ameanza katabia kabaya, akienda shuleni anachelewa kurudi wakati si kawaida yake, tukasema kuna jambo linaendelea kwake,” alisema mzazi huyo.
Akidhibitiwa baad ya kufumaniwa.
USHUSHUSHU
Kwa mujibu wa mzazi huyo aliyeonekana kufura kupita tafsiri ya neno lenyewe, alianza kibarua cha ushushushu kama si upelelezi wa kumfuatilia binti yake ambapo siku moja aliifanyia udukuzi simu yake na kukuta ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenye simu hiyo ukimtaka afike kwenye gesti hiyo.
MBALI NA UJUMBE
Ikadaiwa kuwa, mbali na SMS hizo, mama huyo aliwahi kumsikia binti yake akiwa hewani na ‘mheshimiwa’ huyo jambo lililozidisha hasira zake kama mama akiamini kuna mwanaume anamharibu binti yake aliye na malengo naye mazuri siku za usoni.
Mfanyabiashara na denti huyo wakijutia kwa kitendo walichokifanya.
BINTI ATII AMRI YA WAZAZI
Ndipo mama huyo akamuweka kikao kifupi binti yake na kumtaka aseme ukweli kuhusu mtu aliyemuita gesti Kimara-Suka.
NI KAMA WALISEMA
“Mtu gani mama?”
Mama: “We’ usinitanie, nimekuta meseji kwenye simu yako, kuna mwanaume umemsevu kwa jina la Sweet, amekuita gesti, ni nani?”
Binti: “Aaah! Ni mzee mmoja hivi.”
Mama: “Anaitwa nani?”
Binti: “Anaitwa mzee Beno.”
Mama: “Ni mpenzi wako?”
Binti: (moyoni) “mama bwana, sasa si umeona nimemsevu Sweet anaweza kuwa mjomba ‘angu kweli? (kwa sauti) “ndiyo mama lakini sijawahi kufanya naye chochote hata siku moja.”
Mama: “Apia.”
Binti: “Hakyamungu vile.”
MTEGO
Ikadaiwa kuwa baada ya hapo, binti akatakiwa kumjibu mzee huyo kwamba anakwenda wakutane huko gesti ili wamalizane kwani ‘amemmisi’ sana siku hiyo, mzee akashindwa kujiongeza.
Binti akiwa na mzazi wake na skwadi nyingine walianza safari ya kwenda Kimara –Suka kwenye gesti hiyo ambapo walikaa baa ya jirani, binti akaenda ndani ambako mzee huyo alishafika zamani gani na kumsubiri.
Post a Comment