Uhasama kati ya maafisa polisi na watu weusi umeonekana kuendelea kushika kasi baada ya kijana mmoja mweusi kuripotiwa kuuwawa kwa kupigwa risasi na afisa polisi usiku wa jana(Dec.23) kwenye kituo kimoja cha gesi kilichopo eneo la Berkeley, Missouri nchini Marekani.
Vyombo vya habari vimemnukuu msemaji wa Idara ya polisi wa St.Louis, Sajenti Brian Schellman katika taarifa yake akisema afisa huyo wa polisi alikuwa katika kituo cha gesi kilichopo katika kitongoji cha St.Lousna alipogundua akifuatwa na watu wawili, mmoja wao akidaiwa kuwa na silaha mkononi , afisa aliwafyatulia risasi na kumuua kijana uyo hali iliyopelekea mwenzake kutimua mbio.
Wakati polisi wakikataa kutaja jina la muhanga wa tukio hilo, mwanamke ambaye alitambuliwa na vyombo vya habari kwa jina la Toni Martin alikiambia kituo cha NBC kuwa marehemu ni mtoto wake wa kiume anayeitwa Antonio Martin mwenye umri wa miaka 18 na kudai mwanae alitoka kwenda kumtembelea mpenzi wake.
”Aliondoka nyumbani kwenda kumuona mpenzi wake. Labda alianza kukimbia na wao wakampiga risasi”, alisema Toni na kuongeza kwamba hafikirii kama mtoto wake alibeba silaha.
Toni martin alisema mpenzi wa mtoto wake ndiye aliyemjulisha kuhusu shambulio la risasi na kumpeleka eneo la tukio na kukuta maandamano makubwa ya Raia wakipinga vikali mauaji hayo.
Hivi karibuni kumekuwepo na mfululizo wa matukio ya vifo vya watu weusi kuuwawa kwa kupigwa risasi na maafisa polisi wazungu nchini marekani hali inayopelekea kuchochea vitendo vya kibaguzi na uhasama mkubwa baina ya matabaka mawili.
Miongoni mwa vifo vya watu weusi vilivyowahi kuvuta hisia za watu wengi nchini humo ni pamoja na kifo cha Trayvon Martin, Eric Garner, Mike Brown na kijana Ismaaiyl Brinsley aliyejitoa muhanga kwa kuwauwa kwa risasi maafisa wawili wa polisi na kisha mwenyewe kujimaliza mjini Brooklyn.
Post a Comment