Alizaliwa tarehe 12 Oktoba, 1950 kijiji cha Kagabiro, Wilaya ya Muleba, mtoto wa 5 kati ya watoto 11 wa wakulima, Hayati Ta Alexander Kajumulo na Ma Aulelia Teyolekererwa Rwakajuga (yu hai).
Alisoma Shule ya Msingi ya Kaigara, 1958 -1961. Alifaulu akiwa wa kwanza kwenda Shule ya Kati (Middle School) ya Wasichana ya Kashozi – Kamukukubwa, 1962 -1965 (sasa ni Sekondari ya Wasichana, Hekima). Alifaulu tena akiwa wa kwanza kujiunga na shule ya Sekondari ya Wasichana ya Rugambwa, Bukoba, 1966 – 1969.
Alisonga mbele na kujiunga na kidato cha tano Shule Bingwa ya Wasichana ya Marian College (sasa Kilakala), Morogoro. Mwaka 1972 alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa, Operesheni Tumaini, Ruvu (akiwa pamoja na Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete). Akafaulu tena na kujiunga na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Kitivo cha Kilimo, Morogoro 1972 - 1975.
Alihitimu akiwa ameongoza darasa lake na kupewa nishani ya Mkuu wa Chuo kwa ushindi huo. Aliajiriwa kama Mhadhiri Mzaidizi, Idara ya Uchumi. Mwaka huohuo (1975), alichaguliwa kwenda kusoma masomo ya juu Chuo Kikuu cha Cornell Marekani lakini Desemba 1975 akaamua kufunga ndoa na mchumba wake aliyekuwa amemsubiri siku nyingi amalize masomo, Hayati Balozi Wilson KamuhabwaTibaijuka, aliyekuwa kwa wakati huo Afisa katika Ubalozi wa Tanzania, Stockholm, Swideni.
Katika ndoa yao walijaliwa watoto wanne, Muganyizi (1976), Kemilembe (1979), Kagemulo (1986) na Kankiza (1991). Waliishi vyema hadi Mungu alipowatenganisha Mei, 2000.
Hapa ndipo alipozaliwa na kukulia.
Hapa akiwa na familia yake Moscow ubalozi wa Tanzania
Uzio wa shamba lake huko Muleba,kiasili zaidi.
Geti la kuingia kwenye nyumba yake likiwa limetengenezwa kwa mbao na makuti.
Upande wa mbele wa mjengo wa Mama Tibaijuka
Jasiri haachi asili,kwa mbali kahawa zikiwa zimeanikwa ili zikaushwe kwa jua.
Lango kuu la kuingia ndani ya nyumba
Mandhari nzuri ya nyumba ikiwa imepambwa kwa migomba yenye ukijani.
Post a Comment