Taarifa niliyoisikia kutoka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA kuwa wameridhia KATIBU mkuu wetu Dr Slaa, kupumzika kwa mda usio julikana. Kiukweli nimeumizwa na kusikitishwa kwa uamuzi huo wa Dr Slaa hasa nikikumbuka taabu na mateso aliyoyapata katika kukikuza na kukisimamia leo anaamua kuacha kwa namna alivyo amua kufanya.
Naomba nitumie fursa hii kumuomba mh:Dr Slaa fikiri mara nne ni maumivu makali kiasi gani utakuwa umeyasababisha kwa watanzania wenzako na hasa tunao kuunga mkono na kutambua umuhimu wako na mchango wako ndani ya chama cha CHADEMA na UKAWA kwa ujumla tafadhari nakuomba rejea kambini kwa masilahi ya chama na Taifa.
-JF
Post a Comment