MKE wa Rais wa Marekani Barack Obama, Michelle Obama juzi Jumatatu alitoa shoo ya nguvu kwa kucheza wimbo wa Mark Ronson uitwao "Uptown Funk" akiwa sambamba na mastaa wa "So You Think You Can Dance".

Michelle alikuwa akisherehekea bethidei ya miaka mitano ya kampeni yake ya "Let's Move!" yenye lengo la kuondoa vitambi kwa watoto nchini Marekani.

Michelle alianzisha kampeni hiyo mwaka 2010 baada ya kuwepo watoto wengi wenye vitambi. Mwaka 2012, iligundulika kuwa theluthi moja ya watoto nchini Marekani walikuwa na vitambi au uzito uliopitiliza.
Author Name
Author Description!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment