Akiuzungumzia mjengo huo baada ya kuuona, mkandarasi mmoja ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, alithibitisha kuwa mjengo huo unafikia sh. mil. 400 kwani umechukua nafasi kubwa, na ‘material’ yaliyojengea ni ya gharama.
”Ukitazama kwa makini, material nyingi zilizotumika kwenye ujenzi ni zile ya daraja la juu na si hizi za kawaida ambazo watu wengi wamezoea kujengea,” alisema mkandarasi huyo.Jitihada za kumpata Diamond ili aweze kuzungumzia gharama halisi za mjengo huo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa.
Februari mwaka 2013, nyumba hiyo ikiwa haijakamilika kwa maana ya kupambwa nje na ndani, Diamond alisema imemgharimu sh. mil. 260.Diamond aliripotiwa kuhamia kwenye nyumba hiyo wiki iliyopita, habari za uhakika zinasema kuwa nyota huyo alipata mkosi namba moja baada ya sehemu ya uzio wa upande mmoja kuanguka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Post a Comment