Magazeti hayo yaliandikwa kuwa Nyalandu na Aunty walikutana nchini Marekani kwenye hafla ya ubalozi wa Tanzania nchini humo.
Akiongea kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Ijumaa hii, Nyalandu amedai kuwa hilo ni jambo ambalo alipenda mno kulitolea ufafanuzi kwakuwa lilipoandikwa watu wake wa karibu walimuuliza pia kutaka kufahamu kama kuna ukweli wowote.
“Unajua mpaka nikaanza kucheka,” alisema Nyalandu.
“Unajua watu wana midomo, watu wanaweza wakachonga lakini michongo mingine inaweza ikawa haina deal kabisa.
Pili hata kwa anayechonga pia anajua anasababisha zogo ambalo anataka lizae matunda na wanajaribu kuliendeleza, unaona wanaliamplify, story ambayo haipo wanaipeleka,” aliongeza.
“Mimi nilifika kama mgeni rasmi kwenye tukio ukiwa mwaliko wa ubalozi na tukio lile lilichukua saa moja na huyo dada anayeitwa Aunty Ezekiel katika maisha yangu nimemuona siku moja, ndo hiyo hiyo siku nimemuona, nilikuwa sijawahi kumuona tangu nizaliwe.
Tumekutana naye yeye akiwa mwalikwa pamoja na madj wengine wa Bongo Flava katika tukio lenye watu wengi watanzania katika nchi ya America.
Mimi nikiwa mgeni rasmi nikatoa vyeti, nikatoa hotuba wakanisindikiza nikaondoka. Kwahiyo kwanza katika hiyo situation ya kuwa America atakuwa aliniona kwa saa moja katika ule mkutano lakini pia nilikuwa sijawahi kumuona katika maisha yangu na sijawahi kumuona tena, yaani ni mtu ambaye sifahamiani naye.
Kuna wasichana wengi sana ambao nilishakula nao dinner, tunakutana nao kwenye chai, yaani hao tu ndio ingebidi waseme. Lakini huyu binti hata namba yake ya simu sijawahi kuwa nayo hata hapa ninapozungumza,” alisisitiza.
“Kwanza waliandika kwenye gazeti moja nafikiri ni Jamhuri – lile gazeti ambalo limeniandika mpaka wino umewaishia, yaani wamekosa cha kuandika. Wakasema kwamba ‘Waziri Nyalandu atumia mamilioni ya fedha za serikali na Aunty Ezekiel akiwa Marekani’.
Ikaja kama sensational story. Tukarijibu kiserikali kwamba sio kweli kwasababu yeye alikuwa na safari yake, mimi na safari yangu na haikuwa na uhusiano, ubalozi wa Marekani wakatoa statement.
Lakini baada ya wiki tatu hasa baada ya kutangaza nia ya kwamba itakapofika saa nategemea kuchukua fomu ya chama cha mapinduzi kugombea uongozi wa nchi yetu, nina matumaini makubwa kwamba saa ya kufanya mabadiliko ya aina fulani ya kiuongozi imefika, saa ya kuiongoza nchi hii kwa wakati tulionao imefika na nina matumaini makubwa tutaungana na watanzania wenzangu kufanya jambo la mbele, sasa ile ndio ikaibua vitu vingine.”
“Wakasema ‘huyo Nyalandu sasa huyo dada Aunty Ezekiel ana mimba’ kwahiyo wakasema ana mimba ya mheshimiwa Nyalandu.
Ukweli ni kwamba siku hizi suala la mimba ilikuwa ni zamani unaweza ukasingiziwa. Siku hizi mimba kuna kitu kinaitwa DNA, hata ukichukua tu damu ya kwako na ya kwake sasa hivi unaweza ukaonesha ni kweli au sio kweli. Hakunaga uongo kama huo siku hizi.”
Nyalandu alilisitiza kuhusu kujenga jamii inayosema ukweli na sio kutunga uongo kitu ambacho ni dhambi itakayokufuata mwenyewe.
Awali mke wake, Faraja alidai kuwa habari hiyo haikumsumbua kwakuwa anamwamini mume wake na kwamba sio habari ya kwanza ya aina hiyo kuisikia.
Faraja aliyewahi kuwa Miss Tanzania alidai kuwa ndoa yao haikutetereka kwa kiasi chochote kufuatia uzushi huo.
“Hazikuleta utofauti wowote,” alisema Faraja. “Uzuri sijui niseme nimekuwa sugu. Maneno mengi yameshasemwa kuhusu uhusiano wetu, kuhusu ndoa yetu, kuhusu mapenzi yetu. Lakini katika huo muda wote tukajifunza kwamba uaminifu na upendo ni kitu muhimu sana.
Mkipendana, mkiaminiana maisha hayatoweza kuwatatiza. Na hata kama nikisikia neno kwa mfano leo hii au hata kesho kwangu mimi kwanza natambua kwamba yeye ni kiongozi wa kitaifa, kiongozi wa nchi yetu na ni kiongozi wa familia yangu kwahiyo jambo likisemwa, mara nyingi sana narudi nyuma na kumwangalia yeye kwa mimi ninavyomfahamu , mimi kama mke wake na naamini kwamba mimi namfahamu vilivyo pengine labda katika wanawake ukiacha mama yake mzazi, mimi hapa ndio ninamfahamu sana kuliko wanawake wote.”
“Kwahiyo yaani hainisumbui na ninamfahamu, ninamuamini, ninamheshimu na ninampenda sana.”
Post a Comment