SI siri tena! Staa wa wimbo wa Ndakushima, Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kwa sasa ameamua kukiri wazi kuwa ananogewa na penzi la Wema Sepetu ‘Madame’.
Akizungumza na paparazi wetu Februari 11, mwaka huu maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Dimpoz alisema anawashangaa sana watu kuendelea kumsakama juu ya uhusiano wake na Madame wakati yeye anafahamu shemeji yake kwa Nasibu Abdul ‘Diamond’ ni Zarina Hassan ‘Zari’ kwa sasa.
“Nashindwa kuelewa kuna watu wamekuwa wakinitumia ujumbe eti Diamond atanimaindi kwa ukaribu wangu na Wema, Diamond atanichukia wakati ninavyojua demu wake kwa sasa ni Zari? Niwaambie tu ukaribu wa mimi na Wema ulianza tangu zamani alipokuwa na Diamond,” alisema Dimpoz.
Wakiwa kwenye pozi la kimahaba.
Mahabati ya Dimpoz na Wema yalianza kuonekana laivu juzikati wakati wawili hao walipokuwa nchini Afrika Kusini wakidai kuna ‘project’ ya ngoma mpya ya mwanamuziki huyo waliyokuwa wakiifanya kisha picha zilizowaonesha wakiwa kimahaba zikavuja na kuzua gumzo mitandaoni.
Post a Comment