Mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarab nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yusuph anatarajia kuoa tena mke wa tatu hivi karibuni huku wake zake wawili wakiwa kwenye bifu zito wakitupiana vijembe mtandaoni. Akipiga stori na Uheard na Soudy Brown alisema kuwa anatarajia kuoa mke huyo ambaye anaishi huko visiwani Pemba,na kwamba mipango
ikiwa tayari kila kitu kitakuwa hadharani. Hivi karibuni wake zake wawili ambao ni Malkia Leila Rashid ambaye pia ni mwimbaji wa kundi hilo na mke wake mdogo aitwaye Chiku wamekuwa wakirushiana vijembe kwenye mtandao wa kijamii wa ‘Whatsap’ kwa kuandikiana ‘Status’ za vijembe. Habari zinasema kuwa wake hao wamekuwa kama chui na paka na mzee Yusuph hana mpango wa kuwapatanisha kwa kuwa hakuna hata mmoja aliyeonyesha chuki kwa mwenzake akiwa na nao.
Post a Comment