Featured

    Featured Posts

HIKI NDICHO ALICHO SEMA MAMA YAKE WEMA SEPETU KUHUSU MIMBA YA ZARI WA DIAMOND

SIKU chache baada ya kuvuja kwa picha zinazomuonesha mpenzi wa sasa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na kitumbo kinachoashiria kukua kwa ujauzito, mama mzazi wa zilipendwa wa Diamond, Wema Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu amefunguka kuwa amefurahia tukio hilo.
Mzazi huyo ambaye ni fundi wa kuzungumza, alisema tukio hilo limemfurahisha kwani anaamini ndoto za Diamond kurudiana na binti yake zitakuwa zimeyeyuka rasmi kama alivyokuwa akimuomba Mungu siku zote.
 Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Kuonesha kwamba amefurahishwa na kitendo hicho, alimtaka Zari aendelee kumpenda Diamond, amgande kila idara ili isije kutokea akarudi kwa binti yake ambaye walimwagana mwishoni mwa mwaka jana.
“Yaani kama inawezekana naomba sana huyo Zari azidi kumganda Diamond, asimpe muda wa kugeuka nyuma kabisa ili mambo mengine yaendelee kwa sababu uhusiano wa Diamond na mwanangu haukuwa na baraka zangu,” alisema mama Wema.
Mama Sepetu aliongeza kuwa, hana maana ya kumchagulia mchumba mwanaye bali anahitaji mwanaume yeyote mwenye heshima na anayehiheshimu kwa sababu mwanaume asiyejitambua hawezi kuwa baba bora wa familia.
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akiwa na mama yake, Mariam Sepetu.
“Sio kwamba namchagulia mtoto wangu mume gani amuoe lakini nahitaji mtu mwenye heshima na kujiheshimu mwenyewe ndio anaweza kuwa baba wa familia la sivyo inakuwa ni mambo ya kihunihuni tu kama ilivyokuwa kwa Diamond.”
Alipotafutwa Diamond kuhusiana na kauli hiyo ya mama Wema, simu yake iliita bila kupokelewa lakini kupitia ukurasa wake wa Instagram, staa huyo wa Wimbo wa Mdogomdogo, alitupia picha ya Zari huku akizungushia duara tumboni na kuandika; ‘kileee kinaanza kumharibia mtu mavazi.’
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana