Kundi la
wanamgambo nchini Somalia Al Shabaab limekiri kuwaua watu 36 katika
shambulio lililotokea kwenye machimbo ya kokoto karibu na mji wa Mandera
kaskazini mwa Kenya.
Katika
taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa kundi hilo, wanamgambo hao
wamesisitiza kuwa ndio waliowaua wakenya hao kwa sababu ya majeshi ya
Kenya kuendelea kuwa nchini Somalia.
Taarifa za mauaji hayo zilitolewa kwa mara ya kwanza na Shirika la Msalaba Mwekundu.
Wakazi wa
eneo hilo wamesema waathirika wote wa tukio hilo ni watu wasio Waislam
ambao walikuwa wakifanya kazi katika machimbo hayo yaliyopo Kormey
kilomita 15 kutoka mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya.
Tukio
hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu wapatao 28
waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera.
Kundi la
wapiganaji wa Kiislam la Al Shabab wamekiri kuhusika na mauaji hayo.Mkuu
wa Polisi hilo amesema bado wanafuatilia tukio hilo.
Katika
tukio lingine, mtu mmoja ameripotiwa kuuawa nchini Kenya kufuatia
mlipuko katika klabu moja ya usiku katika mji wa Wajir kaskazini mwa
Kenya.
Kwa
mujibu wa Kamishna wa Polisi wa Wajir, Frederick Sishia, shambulio hilo
limefanyika saa mbili usiku na kuua mtu mmoja na watu wengine wanne
wamejeruhiwa.
Washambuliaji hao walitumia magruneti na silaha nyingine za kijeshi kufanya shambulio hilo.
Wiki iliyopita watu wengi waliuawa eneo la Mandera kaskazini mwa Kenya.
Kenya
imejikuta ikilengwa na mashambulio ya kigaidi tangu majeshi yake
yapelekwe nchini Somalia kukabiliana na wapiganaji wa Al Shabab. Mbali
na miji ya kaskazini mwa Kenya kushambuliwa kila mara, miji mikubwa
nchini humo ya Nairobi na Mombasa imekuwa ikilengwa na mashambulio ya
kigaidi.
Post a Comment