HII kali! Jamaa mmoja ambaye jina lake halikutambulika mara moja, alikutwa amelazwa chini akiwa amelewa chapachapa, maeneo ya Mtaa wa Kongo, Kariakoo jijini Dar, huku kawekewa karatasi kifuani na wahuni ikisomeka; “for sale” (anauzwa).
Kwa mujibu wa chanzo makini, jamaa huyo
alikuwa na mwenzie ambaye inadaiwa kuwa ni kabila moja kwenye gari
ambapo aliposimama maeneo hayo aliwaambia watu kuwa mwenzake huyo
alikuwa amelewa baada ya kufakamia pombe za ofa.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu
kuwa, mwenzake huyo baada ya kuona swaiba wake hajitambui, aliamua
kumshusha maeneo hayo na kumlaza chini kisha kumuwekea karatasi kifuani
iliyokuwa na maandishi yaliyosomeka; “for sale”.
Chanzo kiliendelea kuweka wazi kuwa mtu
huyo alianza kuwaambia watu waliokuwa wamekusanyika mahali hapo kuwa
kama kuna mtu ana shida na ‘mtoto’ anapatikana kwa bei ya maelewano huku
akiwakataza kumpepea.
“Jamaa alizuia watu wasimpepee akidai
kuwa amejitakia kwani haiwezekani mtu upige masanga kiasi cha
kutojitambua,” kilisema chanzo hicho.
Mapaparazi wetu walifika eneo la tukio
na kujionea baadhi ya vijana wa mjini wakitaka kumfanyia kitu mbaya
lakini kuna mzee mmoja aliwazuia.
Post a Comment