Habari za kiuchunguzi za gazeti hili zimebaini kuwa jamaa huyo aliyekuwa na mrembo huyo kumbe anaitwa Kamau Isaack na ni dereva katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Habari hizo zinadai kuwa watu hao walifotoa picha hizo mbaya za kimahaba wakiwa mjini Tanga na hivi sasa zimesambaa jijini Dar es Salaam.
Ilidaiwa kuwa, mara kwa mara mwanaume huyo alikuwa akimuaga mkewe kuwa anasafiri kikazi kumbe alikuwa akiishia kuponda raha na Tuma.
Aidha, imeelezwa kuwa mwanadada huyo sasa anajuta na anahaha kwa kuwa alikuwa akiiba mume wa mtu.
“Unajua huyu jamaa ameajiriwa katika wizara ya mama Sitta ni dereva na amekuwa akisafiri mara kwa mara, lakini haijajulikana kwanini walipiga picha hizi mbaya, ambazo ni kinyume cha maadili,” kilisema chanzo chetu.
Katika uchunguzi uliofanywa na gazeti hili imebainika kuwa mume huyo wa mtu amekuwa si mkaaji sana wa nyumbani kutokana na majukumu mazito ya kikazi yanayomfanya awe safarini mara kwa mara.
Gazeti hili bado linaendelea kufanyia uchunguzi picha zingine ambazo zinatajwa kuwa ni chafu zaidi ambazo haziendani na maadili ya Kitanzania zilizotapakaa mitaani.
Awali, Kamau alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusiana na picha hizo alizikana huku Tuma akisakwa kwa udi na uvumba kupitia simu yake ya mkononi bila mafanikio
Post a Comment