Baada ya East Africa yote kuinua shangwe kubwa siku ya Jumapili Desemba 7 kusherehekea ushindi wa nguvu alioupata Mtanzania Idris kwenye BBAHotshots, kulikuwa na story kwenye mitandao ya kijamii ambazo hazikuwapendeza watu wengi kwani ilionekana kama baadhi ya watu kama Nigeria hawakuwa na amani kuukosa ushindi huo na kuuona ukija Tanzania.
Sasa mpya kutoka Nigeria ni kwamba bilionea mmoja hakupendezwa kumuona mwakilishi wao Tayo akiambulia patupu, bilionea huyo Ayiri Emami amempatia Tayo Folarin pesa ambazo ni zaidi hata ya kiwango ambacho kimetolewa na BBAHotshots kwa mshindi wa kwanza.
Tunawafahamu mabilionea wachache kutoka Nigeria wakiongozwa na Aliko Dangote,Emami leo anakaa kwenye headlines karibu zote za Nigeria kwa kumpatia Tayo dola laki tatu na nusu (350,000/=).
Kiasi hicho ni backup kwa Tayo ambaye alionekana mnyonge sana usiku ambao Idris alitangazwa mshindi, hii itampa Amani ya kuendelea maisha na mpenzi wake na mtoto wake mmoja ambaye alizaliwa wakati Tayo akiwa ndani ya Jumba la Big Brother.
Post a Comment