Davido na Pallaso
Kuna taarifa kutoka nchini Uganda kuwa Davido aliyepo nchini humo aliondoka kwenye club ya jijini Kampala baada ya DJ kucheza wimbo alioshirikishwa naDiamond, Number One Remix.
Davido alikuwa akila bata kwenye lounge iitwayo Laftaz ya jijini Kampala na baadaye mood kukatika baada ya kusikia wimbo huo ukichezwa. Mtandao wa BigEye Uganda umeandika kuwa Davido aliyekuwa amepewa kampani na msanii wa Uganda ambaye pia ni mdogo wake na Jose Chameleone, Pallaso, alirudi kwenye hoteli aliyokuwa amefikia.
Bongo5 imemtafuta Pallaso na haya ndio aliyetuambia: I don’t know, I missed that party, we were already partying and I was not really paying attention so I don’t know,” Pallaso ameiambia Bongo5.
Hata hivyo Pallaso amekiri kusikia uvumi huo.
“I heard some stories but you know there is a lot of gossip going on in Kampala so you could never know what to trust and what not to trust, but I did not really see that part,” ameongeza.
Pallaso amemshirikisha Davido kwenye wimbo wake utakaotoka wiki ijayo.
Post a Comment