90% Huenda mshiriki kutoka Tanzania anayewakilisha ndani ya mjengo waBig Brother ‘hotshots’ , Idris Sultan akaibuka kidedea leo usiku katika shindano hilo.
Tangu asubuhi Runinga ya DStv kupitia Channel 197 na 198 inayoonyesha moja washiriki 8 waliobakia katika mjengo huo, huku kamera ikimmulika zaidi Idris mara kwa mara jambo linaloashiria huenda Watanzania tukacheka kwa ushindi mnono hapo baadaye.
Fainali za Big Brother ‘hotshots’ zinategemewa kufanyika leo Usiku huku Idris akiwaongoza wenzake saba ambao ni Tayo (Nigeria), JJ (Zimbabwe), Nhlanha (Afrika Kusini), Sipe (Malawi), Butterfly (Zimbabwe), Ma mbea (Ghana) pamoja na Macky2 wa Zambia.
Endelea kupigia kura Idris ili leo arudishe heshima Tanzania kwa kunyakuwa kitita cha dola 300,000 (Sawa na 510,186,000).
Ili kumpigia kura Idris nenda sehemu ya kuandikia meseji katika simu yako kisha andika neno VOTE acha nafasi kisha andika IDRIS na tuma kwenda namba 15426. Kura yako ni muhimu sana kwa siku ya leo.
Post a Comment