Ingawa mwenyewe amekuwa akikanusha kila kukicha, mrembo tajiri mwenye maskani yake nchi jirani ya Uganda na Afrika Kusini, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady, anadaiwa kuwa na mtungo mrefu wa wanaume ambapo kama ni kweli anatoka na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ basi jamaa huyo atakuwa anashika nambari 13.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady.
Kwa mujibu wa jarida la linalodili na
habari za showbiz (biashara ya shoo) la E-Vibe la nchini Uganda la hivi
karibuni, Zari ambaye wikiendi iliyopita alimng’arisha Diamond katika
zulia jekundu kwenye Tuzo za Channel O (Choamva) zilizofanyika
Johannesburg nchini Afrika Kusini ‘Sauz’, anadaiwa kuwa ‘klozi’ na idadi
hiyo ndefu ya wanaume.
Zari akiwa amebeba tuzo za Diamond nchini Afrika Kusini.
Jarida hilo lilieleza kwamba ndani ya
kipindi cha miaka 14 baada ya kutimiza umri wa mtu mzima wa miaka 18,
Zari mwenye umri wa miaka 32 sasa, ameshajiachia na wanaume wa kada
mbalimbali wakiwemo vigogo serikalini, wafanyabiashara, mastaa wa tasnia
mbalimbali na hata vijana wadogo.
MABUSUKabla ya Diamond, picha za Zari zilivuja akiwa anabusiana kwa hisia na mwanaume, Farouk Sempala anayesifika kwa dili za mjini. Mara nyingi, Zari amekuwa akishangaza watu na kuacha maswali kuwa nini huwa kinamsukuma kumzoea mwanaume haraka na kuingia naye kwenye urafiki?
Zari au The Boss Lady akiwa na aliyekuwa mumewe Ivan Semwanga.
Kwa mujibu wa jarida hilo, kuna mtandao
maalum wa kundi la watu uliundwa kwa ajili ya kufuatilia nyenendo za
Zari katika sekta ya mapenzi ndipo data zikamwagwa.
MUMEWE
Jarida hilo liliweka wazi baadhi ya wanaume walioko kwenye listi hiyo kuwa ni pamoja na mumewe, Ivan Semwanga ambaye alizaa naye watoto watatu kabla ya kumwagana mwaka jana bila talaka.

STAA WA KIKAPU
Mwingine anayetajwa kwenye listi hiyo ni Isaac Lugudde ambaye ni staa wa mpira wa kikapu nchini Uganda. Hata hivyo naye hakudumu naye.

MIKONONI MWA MTOTO WA MJINI
Lilidai kwamba baada ya Zari kuondoka kwa mumewe Semwanga na kumwacha na watoto nchini Afrika Kusini, mwanadada huyo aliangukia kwenye penzi la mtoto wa mjini nchini Uganda, Farouk Sempala ambaye aliposikia tetesi kuwa anatoka na Diamond ndipo akatangaza kuachana naye.

WENGINE
Wengine waliotajwa katika jarida hilo ni pamoja na Jenerali Jeje Odong, wasanii wa muziki, Mozed Radio na Weasel. Katika listi hiyo ndefu pia wamo Aziz Azion, Isaiah, Robert Ogwal a.k.a Rasta Rob, Exodus, Dj Shiru, mfanyabiashara wa Nigeria na sasa ni zamu ya Diamond.

Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady akiwa na Farouk Sempala.
DIAMOND NA ZARI
Awali walianza kama utani ikisemekana kwamba kuna ‘projekti’ wanaifanya kwa kuwa wote ni mastaa wa Afrika Mashariki.

Hata hivyo, kwa kadiri siku zilivyosonga
mambo yakazidi kuwa hadharani na sasa kila kitu kipo wazi na kwamba
kama hujui kusoma, angalia picha wanavyojiachia kama baba na mama.
Wakiwa nchini Afrika Kusini wikiendi iliyopita, Zari anadaiwa kujitambulisha rasmi kwa mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ ambapo walikuwa beneti hadi watu wakawa wanamsifia Zari kwa kujua umuhimu wa mama mkwe na kumhudumia vizuri.

ZARI ANASEMAJE?
Kwa kuwa kila tukimuuliza Diamond ana uhusiano gani na Zari amekuwa akichenga, kwa upande wa mwanadada huyo amekuwa akichekacheka na kudai wapo kikazi zaidi huku akimsifia jamaa huyo kwenye mitandao ya kijamii.

TATIZO UMRI
Kwa mujibu wa makabrasha ya gazeti hili, Diamond ana umri wa miaka 25 wakati Zari ana miaka 32 hivyo amemzidi kwa miaka 7 hivyo kuonekana ‘anambemenda’ Mbongo Fleva huyo.

WATOTO
Mwanadada Zari ana watoto watatu aliozaa na mumewe, Semwanga huku Diamond akiwa hana hata wa kusingiziwa (kama yupo mwenye mtoto wa Diamond ajitokeze).

WEMA AMWITA DIAMOND KAKA
Tofauti na walivyozoea kuitana ‘Baby’, siku hizi upepo umebadilika kwani aliyekuwa mwandani wa Diamond, Wema Isaa Sepetu amekuwa akimwita jamaa huyo kaka, siku alipompongeza kwa ushindi huo na hivyo kuibua maswali ya kufa mtu.

WABONGO WATAKUNYIMA MSOSI SI MANENO
Wakizungumzia uhusiano wa Diamond na Zari, Wabongo waliozungumza na gazeti hili walionekana kugawanyika.

Wapo waliodai kuwa mwanamama huyo
haendani na Diamond kwa kuwa umri umeenda lakini wapo wanamsifia jamaa
huyo kwa kufanikiwa kumnasa Zari mwenye umbo bomba, mrembo ambaye fedha
zimemtembelea.
Post a Comment