Kweli umbea ndio unaendesha mitandao ya kijamii hapa Bongo.Baada ya ile picha ya zamani ya muigizaji Elizabeth Michael aka Lulu akiwa na mshindi wa BBA 2014, Idris, kupewa vichwa vya habari kuwa mwandada Lulu ameamua kujiweka au kuandaa mazingira ya kuwa karibu na mshindi huyo ili wazipukutishe DOLLAR, eti kisa Lulu aliweka picha hiyo mtandaoni nawatu bila kujiuliza mara mbili wamekuwa wa kiachia comment za ajabu ajabu.
Muda huu tena imeibuka picha hii nayo pia ni yazamani, ya muigizaji Wema Sepetu akiwa na Idris, na sasa inapewa vichwa mbali mbali kwenye blogs na social networks vikionyesha kuwa bwana Idris aliwahi kuwa na mahusiano na Wema, au Wema atamyemelea jamaa, mara hivi mara vile nawatu kutoa maneno makali kumuandama Wema bila hata kuchukua sekunde tano tu kufikiria.
Ukweli ni kwamba hizi ni picha tu, tena ni zamani kabla hata jamaa aja SHINE na hata ukiziangalia kwa undani zote hizi za kawaida tu. Kikubwa ambacho kingepewa kipaumbele ni kuwashukuru wote Wema pamoja na Lulu na mastaa wengine wengi tu wa hapa Tanzania kwani walikuwa wakimuombea kura kwa mashabiki wao wakati wote Idris alipokuwa kwenye jumba la BBA. Na sio kuanza kuzusha habari nyepesi nyepesi kama hizi na kuwarushia maneno machafu.
Post a Comment