Featured

    Featured Posts

SERIKALI IMETENGA PESA ZAIDI YA BILIONI MBILI KWA AJILI YA ELIMU YA KATIBA - IKULU


mKurugenzi ya Mawasiliano Ikulu leo imekiri kuwa Serikali imetenga pesa kwa ajili ya kusambaza uelewa kwa wananchi kuhusu Katiba Inayopendekezwa kupitia vyombo vya habari (Radio, TV, Magazeti n.k). Mkurugenzi wa kitengo hicho Bwana Salva Rweyemamu amekiri kuwa waraka uliotangzwa hivi karibuni na Katibu wa UKAWA Dkt Wilbroad Slaa ni wa kweli, na wala siyo wa siri, na kwamba pesa hizo ni kwa ajili ya kutolea Elimu na si kupigia kampeni Katiba Inayopendekezwa. Juzi Jumanne Tarehe 4 Novemba, 2014, Katibu wa UKAWA Dkt Wilbroad Slaa, alidai kuwa amekamata Waraka wa Siri kutoka Ikulu unaoonesha kuwa Serikali imetenga zaidi ya Shilingi Bilion 2.5 kwa ajili ya kupigia kampeni kwa wananchi Katiba Inayopendekezwa kupitia vyombo vya habari, ili wananchi waikubali.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana