Featured

    Featured Posts

MISS TANZANIA MPYA LILIAN KAMAZIMA AFUNGUKA KUHUSU KUMRITHI SITTI MTEMVU!

Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza kujiuzuru kwa Sitti Mtemvu aliyekua Miss Tanzania 2014 baada ya kuzuka Sintofahamu kuhusu Umri wake, Lundenga amesema Sitti Mtemvu aliandika barua ya kujivua taji na kuiwasilisha kwa kamati ya Miss Tanzania Novemba 5 2014 ambapo kamati hiyo imeridhia kujiuzulu kwake na kumvua taji.Hivyo taji hili na majukumu ya Miss Tanzania sasa yatachukuliwa na mshindi wa pili Lilian Kamazima aliyekaa kushoto katika picha ambaye taratibu za Miss Tanzania zinamruhusu kuchukua jukumu hilo, Hashim Lundenga ametangaza uamuzi huo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya JB Belmonte jijini Dar es salaam leo.

Miss Tanzania 2014 Lilian Kamazima akizungumza na waandishi wa habari kuelezea furaha yake baada ya kamati ya Miss Tanzania kumvisha taji hilo kutokana na kujiuzuru kwa Sitti Mtemvu aliyekuwa Miss Tanzania, Kulia ni Hashim Lundega Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania.
Hashim Lundega Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania akionyesha barua iliyowasilishwa kwa kamati hiyo na Bi. Sitti Mtemvu mara baada ya kujiuzulu Umiss Tanzania na kujivua taji hilo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Total Pageviews

Copyright © DAILY MAIL | Designed By Code Nirvana